Simba SC, Al Ahly zatoka sare 2-2 michuano ya AFL

DAR ES SALAAM-Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam imeandika historia mpya ya soka baada ya kutunishiana misuli na miamba wa soka Al Ahly ya Misri katika uzinduzi wa michuano ya African Football League (AFL).

Ni kupitia mtanange wa nguvu ambao umepigwa Oktoba 20, 2023 katika Dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Simba SC ambao walikuwa ni wenyeji katika mchezo huo wa kwanza wa Robo Fainali ya Ligi ya Soka Afrika (AFL) wamekuwa wa kwanza kuifungua michuano hiyo mipya barani Afrika huku wakitoka sare ya mabao 2-2.

Mabao ya Al Ahly yalifungwa na Reda Slim dakika ya 45+1 na Mahmoud ‘Kahraba’ Soliman dakika ya 63, wakati ya Simba SC yamefungwa na Kibu Dennis dakika ya 53 na Sadio Kanoute dakika ya 59.

Aidha, klabu hizo zitarudiana Jumanne katika Dimba la Cairo International nchini Misri na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati ya Petro de Luanda ya Angola na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini.

Awali, Kocha Mkuu wa Simba SC, Roberto Oliviera ‘Robertinho’ aLIsema ingawa huo utakuwa ni mchezo kutokana na ubora na uzoefu wa Al Ahly hawakua na presha.

“Ni mechi kubwa, Al Ahly ni timu bora na ina uzoefu kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini mpira ni sasa na tupo tayari kwa dakika 90,”alisema Robertinho.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news