Simba SC yatinga hatua ya makundi Afrika

DAR ES SALAAM-Licha ya sare ya kufungana bao moja dhidi ya Power Dynamos kutoka Zambia katika mchezo wa marudiano wa Ligi ya Mabingwa barani Afrika, Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam imefanikiwa kutinga hatua ya makundi.


Mafanikio hayo wameyapata leo Oktoba 1, 2023 katika Dimba la Azam Complex lililopo Kata ya Chamanzi, Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Simba SC imeingia hatua hiyo kwa bao la ugenini kufuatia sare ya mabao 2-2 katika mchezo wa kwanza uliopigwa Uwanja wa Levy Mwanawasa nchini Zambia, Septemba 16, mwaka huu.

Andy Boyeli aliwapatia Power Dynamos bao la kwanza dakika ya 16 kwa shuti kali nje ya 18 lililomshinda mlinda lango Ayoub Lakred.

Baada ya bao hilo, Simba SC walirudi mchezoni kutaka kusawazisha, lakini Power Dynamos walirudi nyuma kuzuia na kufanya mashambulizi ya kushtukiza.

Hata hivyo, dakika ya 68, Simba SC waliopata bao la kuwasazisha baada ya mlinzi Kondwani Chiboni kujifunza akiwa katika jitihada za kuokoa mpira wa krosi uliopigwa na nahodha, John Bocco.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news