TRC yalipa fidia kwa wananchi 250 wanaopitiwa na Reli ya SGR

DODOMA-Shirika la Reli Tanzania (TRC) limelipa fidia kwa wakazi ambao maeneo yao yamepitiwa na mradi wa reli ya kiwango cha kimataifa - SGR kipande cha pili Morogoro - Makutopora Oktoba, 2023

Wananchi takribani 250 wamelipwa fidia katika Wilaya ya Dodoma Mjini, Bahi, Mpwapwa na Chamwino jijini Dodoma, wananchi wengine waliolipwa fidia ni wa Wilaya ya Kilosa na Mvomero mkoani Morogoro na bandaye walilipwa fidia wananchi wa Wilaya ya Manyoni mkoani Singida.

Afisa Ardhi kutoka TRC, Benlulu Lyimo amesema, maeneo yaliyolipwa fidia ni kwa ajili ya kupisha ujenzi wa miundombinu ya umeme na vivuko kwenye reli ya kiwango cha kimataifa.

"Fidia inayolipwa ni kwa mujibu wa Sheria, kanuni na Taratibu za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,"alisisitiza Bi. Benlulu.

Mtendaji wa Kata ya Mkonze Wilaya ya Dodoma Mjini, Bw.Matonya Kaondomo ameishukuru Serikali na TRC kwa kulipa fidia kwa wakati ili wananchi wapishe ujenzi wa miundombinu ya reli ya SGR

"Wananchi wenzangu, fedha hizi mnazolipwa mkanunue maeneo mengine ili muone faida ya mradi,"alisema Bw. Matonya.

Richard Stephen mkazi wa Mtaa wa Muungano B Kata ya Mkonze Wilaya ya Dodoma Mjini ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita kwa kuwalipa fidia kwa kiwango walichokuwa wakikitarajia.

"Eneo langu nilikuwa nalima mazao ya chakula, haya malipo niliyopokea nakwenda kununua eneo lingine," alisema Bw.Richard. Zoezi la ulipaji fidia ni endelevu ili kuhakikisha ujenzi wa miundombinu ya SGR inakuwa ya kiwango cha kimataifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news