Wataalam wa maabara Mtwara waguswa na ufanisi wa MSD

NA DIRAMAKINI

MABORESHO ya huduma za afya upande wa huduma za maabara umeelezwa kusaidia wananchi kupata huduma kwa urahisi na haraka zaidi.

Pia, uwepo wa vifaa tiba vya kisasa, umechagiza kuwezesha vipimo vya sampuli nyingi kwa wakati mmoja. Hayo yamebainishwa kwa nyakati tofauti na wataalam wa maabara kutoka Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mtwara ya Ligula baada ya kupokea mashine za kisasa.

Kutokana na jitihada hizo, wataalamu hao wameipongeza Serikali kupitia Bohari ya Dawa nchini (MSD) kwa kazi nzuri.

Yunus Ijumaa ambaye ni Mtaalamu wa Mahabara katika Hospitali ya Lugula anasema, "Awali tulikuwa tunapima seli mundu zaidi ya saa 24,lakini sasa hivi ndani ya dakika nane,mgonjwa anaweza akapata majibu ya awali na process zingine zikaendelea.

"Kitengo chetu cha Hematology katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Ligula tunaishukuru sana Serikali imetuwezesha kupata mashine kubwa, ambayo ni mashine ya cellblood analyizer, mashine ya hematology ambayo inaturahishia kupima kipimo cha full blood picture ambapo awali mashine kama hiyo haikuwepo.

"Ilikuwa inatulazimu kuwatoa ambao wanauhitaji wa kipimo hicho kutoka hapa kwenda kwa mfano Hospitali ya Ndanda ambako ni umbali mrefu zaidi,lakini kwa sasa hivi kipimo kama hiki kinafanyika hapa hapa kwetu.

"Lakini, pia tunaishukuru Serikali imetupatia mashine ya HP electrolysis, hii ni mashine ambayo inaturahisishia kupima seli mundu, ndani ya dakika nane,awali tulikuwa tunapima selimundu zaidi ya saa 24, lakini sasa hivi ndani ya dakika nane mgonjwa anaweza kupata majibu ya awali na vipimo vingine vikaendelea.

"Uwepo wa mashine hizi umeturahisishia sana kuokoa muda kwenye vipimo vyetu, wagonjwa wetu wanakaa muda mchache zaidi kupata majibu yao tofauti na zamani.

"Tunaishukuru sana Serikali kwa kupitia Bohari ya Dawa (MSD) wametuwezesha kupokea mashine hizi, lakini pia kutuwezesha kupata vitendanishi.

"Kwa mfano mashine yetu ya full blood picture, ni mashine ambayo inatumia reagent, reagent hii isipopatikana kwa wakati ni ngumu kuifanyia kazi.

"Lakini, kwa kupitia MSD wanatuletea reagent kwa wakati. Na pia, pale ambapo mashine zetu zinapata changamoto yoyote,huwa wanakuja mapema, wanawahi mapema kwa ajili ya kufanya matengenezo, wanazifanyia matengenezo kwa wakati,kiukweli tunaishukuru sana."

Reagent ni kitendanishi dutu ambacho kinawezesha majibu, na hutumiwa katika majaribio yanayotumika sana kwa mfano vipimo vya ujauzito, vipimo vya sukari kwenye damu na vifaa vingi vya kupima UVIKO-19.

Naye mtaalamu wa mahabara kutoka hospitalini hapo, Jesca Willium pia ameishukuru Serikali kupitia Bohari ya Dawa (MSD) kwa kuwapatia vifaa ambavyo vina uwezo wa kisasa.

"Ni vifaa vya kisasa ambavyo vina uwezo wa ku-process sampuli na kufanya shughuli nyingi kwa wakati mmoja,inaturahisishia sana kuweza kuhudumia wagonjwa wengi ndani ya muda mfupi, katika Kitengo changu cha Kemia, tumepokea mashine kubwa mbili,zenye uwezo w akufanya sampuli, moja ni sampuni 100 kwa wakati mmoja, na nyingine sampuli 85 kwa wakati mmoja.

"Vyote vikiweza kutoa majibu ndani ya muda mfupi, lakini zaidi tumeweza kupata mashine zingine mbili zenye uwezo wa kufanya testi zaidi ya tano kwa wakati mmoja, kwa hiyo hizi zote zinasaidia kutoa majibu kwa wakati sahihi na ndani ya muda mfupi.

"Mashine ya Architect sf-1 ambayo inapima vipimo vya figo, ini na electro-light kwa ujumla wake, lakini pia tumepokea mashine ya Immunoassay ambayo inatumika kwa ajili ya kupima homoni, homoni zote za uzazi,tyrohid homoni zote tunapimia katika hiyo mashine

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news