Waziri Kairuki ahitimisha Mkutano wa 25 wa UNWTO kwa kufanya ziara Chuo Kikuu Uzbekistan

UZBEKISTAN-Waziri wa Maliasili na Utalii, Mhe. Angellah Kairuki (Mb) amefanya ziara katika Chuo Kikuu cha Utalii na Urithi wa Utamaduni ( International University of Tourism and Cultural Heritage) na kujionea mafunzo yanayotolewa na sambamba na nyenzo za kufundishia.

Akizungumza na Mkuu wa Idara ya Utalii katika chuo hicho leo Oktoba 20, 2023, Mhe. Kairuki ameeleza nia ya kuanzisha ushirikiano kati ya Chuo hicho na Vyuo vya Tanzania vinavyotoa mafunzo ya utalii na ukarimu.

Naye, Mkuu wa Idara ya Utalii wa Chuo hicho, Bw. Akmal Odilov alieleza kuwa ni Chuo cha kimataifa na chenye Wahadhiri wabobezi kutoka mataifa mbalimbali duniani.





Aidha, aliongeza kuwa wako tayari kushirikiana na Tanzania katika kuboresha mitaala, kubadilisha wahadhiri sambamba na wanafunzi kutoka pande zote mbili.

Vilevile, alieleza kuwa Chuo hicho hutoa ufadhili wa Shahada ya Pili katika fani za Utalii na Ukarimu na watatoa kipaumbele kwa Tanzania.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news