Balozi Njalikai akutana na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu

ALIGIERS- Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Algeria, Mheshimiwa Imani Salum Njalikai amefanya mazungumzo na Rais wa Mahakama ya Afrika ya Watu na Haki za Binadamu,Mhe. Jaji Iman Aboud.

Mheshimiwa Balozi Njalikai amefanya mazungumzo na Mheshimiwa Jaji Aboud leo Novemba 19, 2023 katika Ofisi za Ubalozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania jijini Algiers, Algeria.

Mhe. Jaji Aboud anaongoza Mkutano wa 71 wa Mahakama hiyo unaofanyika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Watu wa Algeria kuanzia Novemba 6, 2023 na unatarajiwa kukamilika Desemba 4,2023.Mkutano huo, utakapokamilika unatarajiwa kutoa hukumu ya mashauri takribani tisa ya kimahakama.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news