Mawaziri EAC wakutana jijini Arusha

ARUSHA-Mkutano wa Kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki waanza jijini Arusha.

Mkutano huo umeanza katika Ngazi ya Wataalam wanakutana jijini Arusha kuanzia tarehe 18 - 20 Novemba, 2023 na utafuatiwa na Kikao cha Makatibu Wakuu kitakachofanyika tarehe 21 Novemba 2023, na kufuatiwa na Mkutano wa 44 wa Baraza la Mawaziri utakaofanyika tarehe 22 Novemba 2023.
Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania unaoshiriki katika Mkutano wa kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki ngazi ya wataalamu unaofanyika jijini Arusha tarehe 18 -20 Novemba 2023.
 Wajumbe wa meza kuu wakiongoza Mkutano wa kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki katika ngazi ya Wataalamu unaoendelea jijini Arusha, Mkutano huo unafanyika tarehe 18 -20- Novemba 2023 jijini Arusha utafuatiwa na kikao cha ngazi ya Makatibu Wakuu kitakachofanyika tarehe 21 Novemba na baadaye kufanyika mkutano wa Baraza la Mawaziri tarehe 22 Novemba, 2023.
Wajumbe kutoka katika Jamhuri ya Uganda, Jamhuri ya Rwanda na Jamhuri ya Kenya wanaoshiriki katika Mkutano wa kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioanza tarehe 18 Novemba 2023 jijini Arusha katika ngazi ya Wataalamu.

Mkutano wa ngazi ya Wataalam unapitia na kujadili masuala mbalimbali kuhusu Mtangamano wa Afrika Mashariki ambayo yatawasilishwa katika Mkutano wa ngazi ya Makatibu Wakuu kwa majadiliano kabla ya kuwasilishwa kwenye Mkutano wa 44 wa Baraza la Mawaziri kwa mapendekezo.

Masuala yanayojadiliwa katika Mkutano huo wa wataalamu ni pamoja na Taarifa ya Utekelezaji wa maamuzi na maelekezo ya mkutano cha Baraza la Mawaziri kwa kipindi cha kuanzia tarehe 1 Julai, 2022 - 24 Novemba, 2023; Taarifa ya utekelezaji wa maazimio na maelekezo ya Wakuu wa Nchi wa Jumuiya kuhusu; Majadiliano ya Jamhuri ya Somalia kujiunga na Jumuiya; Hatua iliyofikiwa katika kutafuta Amani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika maeneo ya mchakato wa kijeshi na uongezaji muda wa mkataba wa SOFA; Hali ya Kifedha ya Mfuko wa Akiba wa Jumuiya ya Afrika; majadiliano ya Katiba kuhusu Katiba ya Fungamano la kisiasa Afrika Mashariki; Tathmini ya miswada iliyopitishwa na Bunge la Afrika Mashariki na; Utoaji wa Tuzo kwa washindi wa mashindano ya Uandishi wa insha kwa wanafunzi wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Wajumbe kutoka Jamhuri ya Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wanaoshiriki katika Mkutano wa kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioanza tarehe 18 Novemba 2023 jijini Arusha katika ngazi ya Wataalamu.

Wajumbe wanaoshiriki Mkutano wa kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioanza tarehe 18 Novemba 2023 jijini Arusha katika ngazi ya Wataalamu wakiendelea na kikao.

Wajumbe wanaoshiriki Mkutano wa kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioanza tarehe 18 Novemba 2023 jijini Arusha katika ngazi ya Wataalamu wakiendelea na kikao.

Wajumbe wanaoshiriki Mkutano wa kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki ulioanza tarehe 18 Novemba 2023 jijini Arusha katika ngazi ya Wataalamu wakiendelea na kikao.

Mkutano huo unahudhuriwa na Wajumbe kutoka nchi zote wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki ambazo ni mwenyeji Tanzania, Burundi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) Kenya, Uganda, Rwanda, na Sudan Kusini.

Baada ya kukamilika kwa Mkutano huo wa Kawaida wa 44 wa Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki tarehe 23 Novemba utafanyika Mkutano wa Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi, Usalama wa Chakula na Uendelevu wa Mazingira na kufuatiwa na Mkutano wa kawaida wa 23 wa Wakuu wa Nchi wanachama wa Jumuiya uliopangwa kufanyika jijini Arusha tarehe 24 Novemba, 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news