Benki Kuu yaendelea kuwaelimisha wananchi kila kona

MOROGORO-Novemba 7, 2023 Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imetoa elimu ya utambuzi wa alama za usalama zilizopo katika noti zake kwa wafanyabiashara wa Soko la Chifu Kingalu mkoani Morogoro.
Wananchi hao, wamesema elimu hiyo itawasaidia kutambua noti bandia zilizopo katika mzunguko wa fedha pamoja na kutoa elimu kwa wananchi wengine kwa lengo la kuimarisha sekta ya fedha.

Hii ni sehemu ya kampeni za elimu kwa umma zinazoendeshwa na Benki Kuu katika mikoa mbalimbali nchini ambapo hivi karibuni BoT ilitoa elimu hiyo kwa watumishi wa umma, wadau wa sekta ya fedha na wanafunzi wa vyuo mbalimbali vilivyomo mkoani Singida na Morogoro.

Fahamu

Jukumu la msingi la Benki Kuu ya Tanzania ni kuandaa na kutekeleza sera ya fedha inayolenga kudhibiti mfumuko wa bei na kujenga mfumo wa fedha ulio imara na unaofaa kwa ukuaji endelevu wa uchumi wa taifa.

Majukumu mengine ya Benki Kuu ya Tanzania
  • Kutoa sarafu ya nchi ambayo ni Shilingi ya Tanzania
  • Kusimamia na kudhibiti mabenki na taasisi za fedha
  • Kusimamia na kudhibiti mifumo ya malipo nchini.
  • Kuhifadhi akiba ya nchi ikiwemo fedha za kigeni
  • Benki ya Serikali
  • Benki ya Mabenki; na
  • Kutoa ushauri juu ya masuala ya uchumi na fedha kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news