CMSA yatoa angalizo kuhusu upatu haramu

ARUSHA-Mamlaka ya Masoko ya Mitaji na Dhamana (CMSA) imeitaka jamii kujihadhari na upatu haramu, kwani ni hatari kwa maendeleo yao na Taifa kwa ujumla.
Meneja Uhusiano wa CMSA, Charles Shirima ameyasema hayo jijini Arusha wakati akizungumza kwenye Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa ambayo yanaendelea jijini hapa.

Shirima amesema, jamii ijihadhari na matapeli wanaoahidi watu kuvuna pesa nyingi kirahisi, hivyo waepuke kupoteza pesa ya jasho lao kupitia upatu haramu.

"Kutokana na hali hiyo,Watanzania wanapaswa kujiunga kwenye masoko ya mitaji , kwani ni sehemu ya mfumo wa sekta ya fedha unaowezesha upatikanaji wa fedha kwa ajili ya kugharamia shughuli za maendeleo ya muda mrefu yaani mwaka mmoja,"amesema.

Amesema, fedha za maendeleo hupatikana kwa kuuza hisa za kampuni, hatifungani za kampuni na vipande katika uwekezaji wa pamoja.

Naye Mchambuzi wa Fedha Mwandamizi wa CMCA, Witness Gowelle amesema, kupitia maadhimisho hayo wametoa elimu kwa wajasiriamali mbalimbali ili kuwajengea uwezo zaidi.

"Elimu mbalimbali tuliyotoa kwa wajasiriamali watanufaika nao kupitia masoko ya mitaji ili kujiepusha na upatu haramu,"amesema Gowelle.

Mjasiriamali wa kutoka wilayani Ngorongoro, Sas Kotete amesema wajasiriamali wengi wameathirika kupitia upatu haramu hivyo elimu waliyoipata kutoka CMSA itawasaidia kuepuka hayo.

Mjasiriamali mwingine wa mkoani Arusha, Naini Losusu ameipongeza CMSA kwa kuwapa elimu hiyo kwani inawajengea uwezo zaidi juu ya upatu haramu.

Maadhimisho ya Wiki ya Huduma za Fedha Kitaifa kupitia kauli mbiu ya Elimu ya Fedha,Msingi wa Maendeleo ya Uchumi yanafanyika jijini Arusha, kwa siku sita kuanzia Novemba 20 hadi 26, mwaka huu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news