CWT Halmashauri ya Magu hoi kwa Chuo cha Malya

NA ADELADIUS MAKWEGA

TIMU ya Mpira wa Miguu ya Chuo Cha Maendeleo ya Michezo Malya-Mwanza imeichabanga bila huruma timu ya CWT Halmashauri ya Magu katika mchezo huo uliofanyika katika viwanja vya soka vya chuo michezo Novemba 11, 2023
Mchezo huo wa soka ulitanguliwa na mechi za michezo mingine kadhaa lakini kulingana na hali ya hewa ya mkoa wa Mwanza masika yaliyopamba moto mechi hizo hazikuweza kuendelea.

Mchezo huu wa soka ulianza kwa nguvu ya pande zote kulingana, mashamulizi ya pande zote yalikuwa yakifanyika lakini hakuna upande ulioweza kuliona goli la mwezake. Mchezo huo uliendelea na katika dakika 14 kipindi cha kwanza Adili Othumani Masudi aliliweka kimiani bao la Kwanza la Chuo Cha Maendeelo ya MIichezo Malya.
Goli hilo liliwaibua wanachuo kutoka bwenini na kushangilia goli hilo, huku wenegine wakitumia majembe, ndoo na ngoma kama zana za kutoa milio iliyombatana na maneno ya tambo kama pongezi kwa Adili Othumani Masudi aliyefungulia mlango wa karamu ya ushindi.

Mchezo huo uliendelea sasa timu ya CWT Halmashauri Magu iliongeza nguvu na kusawazisha bao hilo na sasa matokeo uwanjani yakawa moja kwa moja.
Baada ya dakika tano za bao la CWT Magu, Benjamini Paulo wa Chuo Cha Maendeleo ya Michezo Malya aliuweka kimia mpira uliopita kando kushoto kwa golikipa wa timu ya CWT Magu na hao Timu ya ChuoCha Maendeloe ya Michezo ikawa sasa ipo Karamuni.

Shangwe ziliongezeka na kuwavuta kiwanjani wakazi wengi wa Malya na mashabiki hao kuchora umbo la mstatiri likizunguka uwanja huo wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo inayoongozwa na mhe. Dkt. Damas Ndumbaro.
Wakizungumza mara baada ya mechi hiyo kumalizika Kocha Msaidizi wa timu ya soka ya Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya Onesmo Leonard alisema kuwa mechi ilikuwa nzuri na kali. “Tumeshinda lakini hata wenzetu japokuwa wameshindwa, wameonesha mchezo mzuri.”
Wakizungumza na mwandishi wa ripoti hii mwakilishi wa Kiongozi wa CWT kutoka Wilaya ya Magu amesema kuwa hali ya hewa imewanyima furaha kuweza kucheza michezo yote lakini wameburudika kwa kiasi katika mchezo wa soka.

“Sasa tupo katika ziara za kujipima nguvu kwa ajili ya maandalizi ya mashindano ya Siku ya Mwalimu Dunia yanayotarajiwa kuanza juma lijalo na kuhitimishwa Disemba 13,2023 ambapo kitaifa itakuwa kilele ya siku hiyo inayofanyika mkoani Mwanza.”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news