Dkt.Mahera atoa wito kwa maafisa TEHAMA wa halmashauri

DODOMA-Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya Ofisi ya Rais - TAMISEMI,Dkt. Wilson Mahera amewataka maafisa TEHAMA wa halmashauri za Mkoa wa Dodoma kutumia mafunzo wanayoyapata kuleta ufanisi katika utoaji wa huduma za afya kwa wananchi.

Dkt. Mahera ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya Maafisa TEHAMA wa Mkoa wa Dodoma kuhusu mfumo huo Novemba 13, 2023 2023 yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Mkuu wa Mkoa.

Amesema, Maafisa TEHAMA wanapaswa kutumia ujuzi watakaopata kupitia mafunzo haya na kwenda kuwafundisha watumishi wa ngazi za kutolea huduma za Afya kwenye vituo vya kutolea huduma kwa ngazi za Halmashauri.


“Nyie sasa ni TOT (Trainer of Trainees) tujenge uwezo kwa watumiaji wa GOTHOMIS na watumishi wengine katika ngazi zote kwenye vituo vya kutolea huduma pamoja na usimamizi wa karibu na matengenezo ya mfumo huu “ amesema Dkt. Mahera.

GOTHoMIS ni mfumo unaosimaia shughuli za Hospitali Tanzania na unatumika kwenye vituo vya kutolea huduma nchini.Mafunzo ya mfumo huu yametolewa na Ofisi ya Rais - TAMISEMI kwa kushirikiana na KOICA na PMC.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news