Jamii yapewa elimu ya uchaguzi wa nishati za kupikia

MOROGORO-Chuo Kikuu Mzumbe kupitia Mradi wa Elimu ya Juu kwa Mageuzi ya Kiuchumi (HEET), kimeendelea kutoa elimu kwa jamii ili kusaidia kuleta mageuzi chanya ya kiuchumi.

Elimu imetolewa kupitia semina iliyofanyika tarehe 03 Novemba 2023, Chuo Kikuu Mzumbe Kampasi Kuu Morogoro.
Akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina hiyo Dkt. Lohoya Chamwali (kwa niaba ya Kaimu Mratibu wa Mradi wa HEET Chuo Kikuu Mzumbe), ameeleza lengo la semina hiyo kuwa ni kuisaidia jamii katika jitihada ya kupunguza umaskini kwa uchaguzi wa nishati sahihi ya kupikia.

Amesema semina hiyo ni matokeo ya utafiti uliofanywa na Watafiti kutoka Kitivo cha Sayansi ya Jamii chini ya uratibu wa HEET upande wa Kukuza uwezo wa Utafiti na Ubunifu tumishi unaoratibiwa na Dkt. Christina Shitima, na usaidizi wa Kurugenzi ya Huduma za Umma.

Kwa upande wake Mhadhiri Msaidizi kutoka Idara ya Uchumi, Kitivo cha Sayansi za Jamii, Chuo Kikuu Mzumbe na mwezeshaji wa Semina, Bi. Felister Tibamanya aliwasilisha mada kuhusu “Uchaguzi wa Nishati ya Kupikia”. Bi. Tibamanya amebainisha aina za nishati na athari zake ili kujenga uelewa kwa wanasemina.

Aidha, Mhadhiri Msaidizi kutoka Idara ya Mazingira na Maendeleo Endelevu katika Taasisi ya Taaluma za Maendeleo (IDS) Chuo Kikuu Mzumbe na ambae pia ni Mwezeshaji wa Semina hiyo, Bi. Elihaika Joseph aliwasilisha mada kuhusu “Nishati ya Kupikia na Umaskini” na namna nishati isiyofaa inavyoweza kuchangia umaskini.

Kwa upande mwingine Mkufunzi Msaidizi kutoka Idara ya Uchumi, Kitivo cha Sayansi za Jamii Chuo Kikuu Mzumbe, Bi. Nyamsabi Nyamwero aliwasilisha mada kuhusu “Uchaguzi wa Nishati ya Kupikia”. Bi. Nyamsabi alizungumzia kuhusu nishati ambazo ni rafiki wa mazingira, zenye gharama nafuu lakini pia zisizo na madhara kwa afya ya binadamu.





Afisa Mtendaji wa Kijiji cha Changarawe, Bi. Teddy S. Eustach, kwa niaba ya viongozi hao ametoa shukrani kwa Chuo Kikuu Mzumbe kwa kuona umuhimu wa kuandaa semina hiyo. Bi. Eustach ameomba semina hizo kuwa endelevu na kukuza uelewa wa wananchi na kuona umuhimu wa matumizi ya nishati sahihi na itakayosaidia kupunguza umaskini kwa jamii.Karibu Chuo Kikuu Mzumbe, “Tujifunze Kwa Maendeleo ya Watu”

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news