Kazakhstan waonesha utayari kushirikia na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto

NA TIGANYA VINCENT
KAZAKHSTAN

TAASISI ya Mafunzo kwa ajili ya kuwaanda Majaji ya nchini Kazakhstan imesema iko tayari kushirikiana na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto nchini kwa lengo la kubadilishana uzoefu utakaosaidia kuimarisha utendaji na kuwaendeleza Maafisa hao wa Mahakama.

Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel (katikati) akizungumza jana na Uongozi wa Taasisi ya Mafunzo ya Kuwandaa Majaji ya Nchini Kazakhstan wakati wa ujumbe aliouongoza ulipokwenda kujifunza mambo mbalimbali ikiwemo wanavyotoa mafunzo.

Hatua hiyo imefikiwa jana katika mji Mkuu wa Kazakhstan wa Astana wakati mkutano kati ya ujumbe wa Mahakama ya Tanzania uliongozwa na Mtendaji Mkuu Profesa Elisante Ole Gabriel pamoja na ule wa Taasisi ya Majaji ya Mahakama ya Upeo ya Kazakhstan.

Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Majaji ya Kazakhstan iliyopo chini ya Mahakama ya Upeo Baimoldina Zauresh Hamitovna alisema kuwa wao wako tayari kuingia makubaliano na Chuo cha Uongozi wa Mahakama cha Lushoto cha Tanzania kwa lengo la kubalishana uzoefu kitaaluma na kuboresha sekta ya utoaji haki kwa pande zote.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania na Mkuu wa Kitengo cha Maboresho cha Mahakama ya Tanzania Mhe. Dkt. Angelo Rumisha (wa pili kutoka kulia) akitoa ufafanunizi kwa Uongozi wa Taasisi ya Mafunzo ya Kuwaandaa Majaji ya Kazakhstan wakati wa ziara ya mafunzo katika Taasisi hiyo jana.

Alisema kwa muundo wao kabla ya mtu kuwa Jaji anatakiwa kushiriki mafunzo ya Shahada ya Uzamili(Master Degree) ya Sheria katika Taasisi hiyo na ilia pate udahili anapaswa kuwa miaka 28 kuendelea, Stashaha(Diploma) katika fani ya Sheria na uzoefu usiopungua miaka mitano .

Zauresh aliongeza kuwa nchini Kazakhstan kuna njia mbili za kuwa Jaji ,ikiwa ya Kwanza lazima mtu awe amesoma Stashahada(Diploma) ya Sheria katika Chuo Kikuu cha Nchi hiyo na ya pili ni lazima mtu asome katika Taasisi ya Mafunzo kwa ajili ya kuwaanda Majaji na kufaulu mitihani yote
Mkuu wa Taasisi ya Mafunzo ya Majaji ya Kazakhstan iliyopo chini ya Mahakama ya Upeo Baimoldina Zauresh Hamitovna (katikati) akitoa maelezo jana kwa ujumbe wa Mahakama ya Tanzania uliokwenda kujifunza jinsi wanavyowaandaa Majaji kabla ya kuteuliwa.

Alisema mtu anayepitia katika Taasisi ya Mafunzo ya kuwaanda Majaji anakuwa na nafasi kubwa ya kufaulu wakati wa ushindani wa kuwatafuta watu wanaostahili kuteuliwa kuwa Majaji nchini humo.

Awali Mtendaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Prof. Elisante Ole Gabriel aliuomba uongozi wa Taasisi hiyo kuangalia uwezo wa kuingia makubaliano ya kushirikiana na Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto nchini Tanzania katika kubadiliana uzoefu wa kuwaendeleza Maafisa Mahakama na Watumishi wengine.

Alisema kuwa Chuo cha Uongozi wa Mahakama cha Lushoto kimekuwa na utaratibu wa kuwapa mafunzo elekezi, Majaji, Mahakimu na Watumishi wengi wasio Maafisa wa Mahakama kabla ya kuanza majukumu yao mapya , jambo ambalo limesaidia kufanyakazi kwa ufanisi ndani ya Mahakama ya Tanzania.

Prof. Ole Gabriel alisema wakikubaliana wanaweza kuandaa Programu ambazo zinaweza kufundishwa katika pande mbili kama sehemu ya kubadilishana uzoefu na kujngeana uwezo kwa watumishi na Maafisa wa Mahakama waliopo kazini na wale walioteuliwa kuingia kazini.
Alisema endapo watakubaliana , uongozi wa Mahakama ya Tanzania utahakikisha unasimamia makubaliano yaliyofiukiwa kwa manufaa ya pande zote mbili.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Mhe. Dkt. Angelo Rumisha alisema alisema kwa Tanzania Majaji wanaandaliwa kutoka Vyuo Vikuu mbalimbali kwa kupata Shahada ya Sheria na kupita katika Shule Kuu ya Sheria na wanapoteliwa wanapata mafunzo elekezi katika Chuo cha Uongozi Lushoto.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news