Mfalme Zumaridi afungisha harusi ya mtoto wake Daniel Raphel

MWANZA-Maelfu ya waumini wanaoiamini huduma ya kiroho inayoongozwa na Diana Bundala maarufu kama Mfalme Zumaridi wamejumuika pamoja katika sherehe kubwa za harusi ya mtoto wake.

Mtoto wa Mfalme Zumaridi, Daniel Raphel alifungishwa harusi hiyo hivi karibuni na mchumba wake, Penina Thomas katika hekalu la mama yake huyo lililopo huko Mtaa wa Buguku ndani ya Kata ya Buhongwa jijini Mwanza.

Zilikuwa kati ya sherehe ambazo zilitawaliwa na nderemo na vifijo kutoka kwa maelfu ya waumini hao ikiwa ni miezi kadhaa imepita baada ya mama yake Diana (Mfalme Zumaridi) kupitia katika changamoto kadhaa ikiwemo kufunguliwa kesi mahakamani.

Februari 26,2022 Mfalme Zumari na waumini wake 83 walikamatwa nyumbani kwake huko Buguku na kufunguliwa kesi tatu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza.

Watuhumiwa hao walifunguliwa kesi zenye mashtaka tofauti ikiwemo kuzuia maafisa wa Serikali kutekeleza majukumu yao, usafirishaji haramu wa binadamu na kufanya kusanyiko lisilo na kibali.

Mfalme Zumaridi aliachiwa huru Februari 18,2023 baada ya kumaliza kifungo chake cha mwaka mmoja katika Gereza Kuu la Butimba, ambapo mahakama iliamuru atumikie mwezi mmoja gerezani baada ya kukaa mahabusu miezi 11.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news