Mungu ambariki Mtume Dkt.Nyaga kwa moyo wa upendo kwetu-Watu wenye ulemavu wa ngozi

DAR ES SAALAAM-Watu wenye ulemavu wa ngozi (Albino) jijini Dar es Salaam, wamesema wanaisubiria kwa shauku kubwa Desemba 3, 2023 ili wakakutane na mfariji wao,Mtume na Nabii Dkt.Peter Nyaga wa Kanisa la RGC Miracle Centre lililopo Tabata Chang'ombe jijini Dar es Salaam.

Kwa nyakati tofauti wamesema kuwa, siku hiyo Mtume Dkt.Nyaga amewaandalia zawadi na mitaji kwa kila mmoja ikiwa ni utaratibu ambao amekuwa akiufanya kwa zaidi ya miaka 17 sasa.








"Mtume Dkt.Nyaga ni miongoni mwa watumishi wachache sana wa Mungu pengine kwa Tanzania na Afrika kwa ujumla, amekuwa na moyo wa upendo, bila kujali dini ya mtu au imani na itikadi yake amekuwa akitubariki kwa sadaka na vyakula tele.

"Ninaamini tarehe 3 Desemba, 2023 itakuwa ni siku yetu ya kula na kunywa ndani ya Kanisa la RGC Miracle Centre Tabata Chang'ombe jijini Dar es Salaam,"amesema mmoja wa wanawake wenye ulemavu wa ngozi, Bi.Rashida Hassan mkazi wa Kigamboni jijini Dar es Salaam.

Bi. Rashida amesema, kwa miaka minne mfululizo akineemeka kupitia misaada, mitaji na vyakula vinavyotolewa na Mtume Dkt.Nyaga kanisani hapo.

"Awali nilifikiri kwa sababu mimi ninatokea katiak Uislamu nisingepata msaada kanisani kwa Mtume Dkt.Nyaga, lakini nilishangaa sana kuona maelfu ya ndugu zangu wakipatiwa misaada na fedha taslimu kwa ajili ya mitaji ya kuendeshea biashara zao. Ninafarijika sana, Mungu ambariki Mtume Dkt.Nyaga kwa moyo wa upendo kwetu,"amesema Bi,Rashida.

Naye Justin Joseph ambaye ni kijana mwenye ulemavu wa ngozi kutoka Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo amesema, Mtume Dkt.Nyaga amekuwa akiwapatia zawadi bila kujali ni muumini wa kanisa hilo au la.








"Mimi wala huwa siabudu kwa kanisani hapo, lakini pale ninaposikia anagawa misaada ya vyakula na mitaji huwa ninafika na ninapatiwa, jambo la kufurahisha zaidi hata chakula ninakula tena cha kutosha,"amesema Joseph.

Akizungumzia kuhusiana na hilo,Balozi wa Amani Duniani ambaye pia ni Mtume na Nabii Dkt.Peter Njue Nyaga wa Urejesho TV Africa na Kanisa la RGC Miracle Centre lililopo Tabata Chang'ombe jijini Dar es Salaam amesema, bila kujali imani ya mtu au itikadi siku hiyo kila mmoja atapokea baraka.

Mtume na Nabii Dkt.Peter Nyaga amekuwa akitoa misaada kwa maelfu ya wajane, walemavu, vikongwe, yatima na watu wasiojiweza katika kipindi cha miaka 17.

"Na Desemba 2, 2023 nitagawa misaada kwa watu 1,000. Wengine watapewa vyakula, wengine watapewa mitaji ya biashara na vitu mbalimbali, tukio hili la kihistoria litafanyika ndani ya Kanisa la RGC Miracle Centre Tabata Chang'ombe jijini Dar es Salaam.










"Wakazi wote wa Dar es Salaam, msipange kukosa na itakuwa ni siku tatu tarehe 1 itakuwa ni siku ya kongamano, tarehe 2 itakuwa ni siku ya kongamano na tarehe 3 ni sherehe kubwa ambapo chakula cha mchana, vinywaji vitatolewa bure.

"Na wajane, viwete, yaani watu wenye ulemavu wakiwemo Albino, na watu wasiojiweza zaidi ya 1000 watapewa misaada.

"Kama unahitaji kusapoti huduma hii ili tuweze kuwapatia wahitaji wengi zaidi mahitai siku hiyo unaweza kutuma sapoti yako ya sadaka kupitia Tigo Pesa namba 0716 147361 nami Mtume Dkt.Petr Nyaga nitapokea na kukuombea,"amesema Nabii na Mtume Dkt.Nyaga.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news