Neema zaidi zinakuja kwa wajasiriamali-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi amesema mpaka kufikia mwaka 2025 atakuwa ameshatimiza ahadi zote alizozitoa wakati wa kampeni.

Miongoni mwa ahadi hizo ni maeneo mazuri ya kufanya biashara, mitaji pamoja na kodi nafuu katika masoko wanapofanyia biashara zao.

Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo Novemba 2,2023 wakati alipofungua jengo la wajasiriamali Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Vilevile ameleeza kuwa, shilingi bilioni 31 zilizowekwa na Serikali katika Benki ya CRDB wajasiriamali wameendelea kukopa bila ya riba kwa sababu riba zote zinabebwa na Serikali.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amewahimiza wajasiriamali waliokuwa kwenye maeneo rasmi waendelee kuomba mitaji hiyo ya Serikali ambayo haina riba.

Pia ametoa miezi mitatu bure bila kulipa kodi kwa wajasiriamali wa kituo cha Wete, Mkoa wa Kaskazini Pemba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news