Nitagombana na wachache kwa maslahi ya wengi-Waziri Mchengerwa

DAR ES SALAAM-Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mhe. Mohamed Mchengerwa amesema yuko tayari kutofautiana na watumishi wachache watakaokuwa wanakwamisha utatuzi wa changamoto za walimu kwa maslahi ya walimu wengi ambao wanalitumikia Taifa kwa moyo.

Waziri Mchengerwa ameyasema hayo leo Novemba 27,2023 wakati wa hafla ya kukabidhi gari, pikipiki 62 na kompyuya mpakato 159 kwa Makatibu Wasaidizi wa Tume ya Utumishi wa Walimu iliyofanyika kwenye shule ya Sekondari Tambaza mkoani Dar es Salaam.

"Nikiwa Ofisi ya Rais -Utumishi chini ya uongozi wa Serikali ya Awamu ya Sita tuliwapandisha madaraja walimu 227,363 na kuwabadilishia walimu 11,642 lakini katika kufanikisha hili kuna wakuu wa Idara ya Utumishi tuliwaondoa kwenye nafasi zao kwa sababu walikuwa wanakwamisha haki hizi za walimu.

“Sasa nielekeze tena katika kipindi changu sitaki kusikia changamoto za walimu kila mmoja kwenye nafasi yake anayehusika kwa namna moja au kutatua changamoto za walimu awajibike ipasavyo vinginevyo nitamchukulia hatua stahiki.

"Kipindi hiki kitakuwa kigumu kidogo kwa wale wazembe katika kutekeleza majumuku yao, lakini kitakua kizuri kwa wale wanaochapa kazi kwa maslahi ya watanzania.

"Nataka changamoto zote za walimu za kupandishwa madaraja na malimbikizo ya mishahara zikafanyiwe kazi ipasavyo."

Awali akizungumza katika hafla hiyo Katibu wa Tume ya Utumishi wa Walimu, Paulina Mkwama amesema, vifaa hivyo vinavyokabidhiwa leo vitasaidia kuboresha utendaji kazi wa watendaji katika tume, hivyo kuboresha utoaji wa huduma kwa walimu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news