Rais Dkt.Mwinyi ateua viongozi 25 leo

NA GODFREY NNKO

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,Mheshimiwa Dkt.Hussein Ali Mwinyi ameteua viongozi mbalimbali.

Miongoni mwa walioteuliwa ni Khadija Shamte Mzee kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar. Kabla ya uteuzi huo, Khadija alikuwa Mwenyekiti wa Tume ya Kurekebisha Sheria Zanzibar.

Pia, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Haji Suleiman Khamisi (Tetere) kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar. Kabla ya uteuzi huo, Haji alikuwa Wakili wa Kujitegemea.

Tatu, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Salum Hassan Bakari kuwa Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar. Kabla ya uteuzi huo, Salum alikuwa Naibu Mrajis wa Mahakama Kuu.

Nne, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Sheha Makame Mussa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Taasisi ya Nyaraka na Kumbukumbu Zanzibar. Sheha ni mstaafu wa utumishi wa umma.

Tano, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Dkt.Mahmoud Abdulwahab Alawi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Mawasiliano Zanzibar (ZICTIA). Dkt.Mahmoud ni Mkuu wa Taasisi ya Karume ya Sayansi na Teknolojia Zanzibar.

Sita, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Balozi Omar Yussuf Mzee kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Taasisi ya Viwango Zanzibar (ZBS). Balozi Omari ni Waziri mstaafu wa Awabu ya Saba.

Saba, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Mohamed Aboud Mohamed kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Udhibiti wa Leseni za Biashara (BLRC). Mohamed ni Waziri mstaafu wa Awamu ya Saba.

Nane, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Kidawa Hamid Saleh kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Biashara la Taifa Zanzibar (ZSTC).Kidawa ni mstaafu wa utumishi wa umma.

Tisa, Mheshimiwa Rais Dkt.Mwinyi amemteua Akif Ali Khamis kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Mwani Zanzibar (Zanzibar Seaweed Company Limited). Akif ni Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bandari Zanzibar;



Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news