Rais Frank-Walter Steinmeier atembelea Twiga Cement

DAR ES SALAAM-Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier ametembelea kiwanda cha kuzalisha saruji cha Twiga (Twiga Cement) kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam.

Rais wa Ujerumani, Frank-Walter Steinmeier akiangalia taswira ya Kiwanda cha kuzalisha saruji cha Twiga (Twiga Cement) kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam.

Rais Frank-Walter Steinmeier amepata fursa ya kujionea shughuli mbalimbali za uzalishaji saruji zinazoendelea kiwandani hapo.

Kiwanda hicho cha Twiga Cement kinachotarajia kuongeza uwekezaji wake kufikia Dola za Marekani Milioni 500 kilijengwa nchini mwaka 1967.


Rais wa Jamhuri ya Shirikisho la Ujerumani Mheshimiwa Frank-Walter Steinmeier akiangalia moja ya malighafi zinazotumika katika uzalishaji wa saruji alipotembelea Kiwanda cha kuzalisha saruji cha Twiga (Twiga Cement) kilichopo Tegeta jijini Dar es Salaam.

Kiwanda cha Twiga Cement kina ubia na Kampuni ya Scancem International ya nchini Ujerumani.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news