MBUNGE wa Jimbo la Ilemela, Mhe. William Kafiti, amezindua rasmi programu ya Kafiti School Talent, inayolenga kutambua, kukuza na kuendeleza vipaji vya wanafunzi wa shule mbalimbali katika Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.
Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Mhe. Kafiti alisema kuwa vijana wenye vipaji wanahitaji kupewa fursa na mazingira bora ili viweze kuwa chachu ya mafanikio yao na maendeleo ya jamii.
Alisisitiza kuwa programu hiyo itasaidia kuwajengea wanafunzi kujiamini, kuonesha uwezo wao na kufungua milango ya mafanikio katika nyanja mbalimbali za sanaa, michezo na ubunifu.

Tags
Kurasa za Magazeti
Kurasa za Mbele na Nyuma za Magazeti
Magazeti
Magazeti ya Leo
Magazetini
Magazetini leo
Yaliyojiri Magazetini Leo




















