Sekta ya Elimu imeanza mageuzi makubwa-Rais Dkt.Mwinyi

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,DkT.Hussein Ali Mwinyi amesema sekta ya elimu imeanza na mageuzi makubwa ujenzi wa miundombinu kwa Skuli za kisasa za msingi na Sekondari za ghorofa zenye vifaa vya kisasa ikiwemo maabara, vyumba vya kompyuta, vyoo vya kutosha na madawati.
Pia ameeleza kuwa, Serikali inaimarisha mitaala ya elimu, ajira za walimu, kuendelea kutizama maslahi ya walimu na kurekebisha vyuo vya walimu.

Wanafunzi wa Kidato cha nne na sita wanaume na wanawake waliofaulu vizuri katika mitihani yao ya Taifa wakiwa katika hafla ya Chakula cha Mchana kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Hussein Ali Mwinyi jana katika viwanja vya Ikulu ya Pagali Pemba.

Wanafunzi wa Kidato cha 4 na 6 wanaume na wanawake waliofaulu vizuri katika mitihani yao ya Taifa wakiwa katika hafla ya Chakula cha Mchana kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi katika viwanja vya Ikulu ya Pagali Pemba.

Baadhi wa Walimu wa Wanafunzi wa Skuli mbali mbali za kidato cha nne na sita kisiwani Pemba walioshiriki katika hafla ya Chakula cha Mchana kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi jana katika viwanja vya Ikulu ya Pagali Pemba.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi alipokuwa akizungumza na Viongozi,Walimu na Wanafunzi katika hafla ya Chakula cha Mchana alichowandalia Wanafunzi wa Skuli mbali mbali za kidato cha nne na sita waliofaulu vizuri katika mitihani yao ya Taifa jana katika viwanja vya Ikulu ya Pagali Pemba.

Baadhi ya Wanafunzi wanawake wa waliofaulu vizuri katika mitihani yao ya Taifa kidato cha nne na sita walioshiriki katika hafla ya Chakula cha Mchana kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi jana katika viwanja vya Ikulu ya Pagali Pemba.
Baadhi ya Wanafunzi wanawake wa waliofaulu vizuri katika mitihani yao ya Taifa kidato cha nne na sita walioshiriki katika hafla ya Chakula cha Mchana kilichoandaliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi jana katika viwanja vya Ikulu ya Pagali Pemba. .
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi na Mama Mariam Mwinyi (katikati) pamoja na Viongozi wengine wakiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Skuli mbali mbali waliofaulu vizuri katika mitihani yao ya Taifa kidato cha Nne na Sita katika hafla ya chakula walichoandaliwa Wanafunzi hao jana katika viwanja vya Ikulu ya Pagali Pemba.

Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo Novemba 2, 2023 katika hafla fupi ya kuwapongeza wanafunzi waliopata daraja la kwanza kwa kidato cha nne mwaka 2022 na kidato cha sita mwaka huu viwanja vya Ikulu Pagali Pemba.

Vilevile Rais Dkt.Mwinyi ametoa zawadi ya kompyuta mpakato moja kwa kila mwanafunzi aliyefaulu daraja la kwanza ambapo idadi yao ni 1451 wa kidato na nne na sita na kujumuika pamoja nao katika hafla ya chakula cha mchana Ikulu Pagali Pemba.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news