Zanzibar kuanzisha utalii wa mikutano

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Hussein Ali Mwinyi amesema ni fursa muhimu kwa Zanzibar kuwa na utalii wa mikutano na kinachotakiwa kufanyika hivi sasa ni kujipanga kuweka miundombinu mizuri maeneo ya kufanyia mikutano hiyo.
Rais Dkt.Mwinyi amesema hayo Novemba 3, 2023 Ikulu jijini Zanzibar katika mahojiano ya kipindi cha Mizani Exclusive kilichorushwa mubashara kupitia TBC kilichoangazia Miaka Mitatu ya Uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nane Zanzibar.

Aidha, Rais Dkt.Mwinyi amezitaka sekta binafsi kuangalia uwezekano wa kuweka kumbi mbalimbali za mikutano ili kuwezesha kufanyika kwa mikutano mingi, hali ambayo itachangia kuleta wageni na watalii wengi kwa wakati mmoja.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news