Shirikisho la Jamhuri ya Somalia lakubaliwa kujiunga na EAC

ARUSHA-Mkutano wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki umeridhia ombi la Shirikisho la Jamhuri ya Somalia kujiunga na Jumuiya hiyo katika Mkutano wa 23 wa Kawaida wa Jumuiya hiyo uliofanyika jijini Arusha.

Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa kwenye Mkutano wa 23 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.

Mkutano uliopitisha ombi hilo umehudhuriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. William Ruto, Rais wa Jamhuri ya Burundi Mhe. Evereste Ndayishimiye, Rais wa Jamhuri ya Uganda Mhe. Yoweri Kaguta Museveni, Rais wa Jamhuri ya Sudani Kusini Mhe. Silver Kiir, Waziri Mkuu wa Rwanda aliyemwakilisha Rais Paul Kagame na Makamu Rais wa DRC aliyemwakilisha Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Mhe. Antonie Tshisekedi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia kwenye Mkutano wa 23 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.

Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye ambaye amemaliza muda wake wa Uenyekiti wa Jumuiya ya Afrika Mashariki akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti Mpya wa Jumuiya hiyo Rais wa Sudan Kusini Mhe. Salva Kiir Mayardit wakati wa Mkutano wa kawaida wa 23 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliofanyika jijini Arusha.

Viongozi mbalimbali wakifuatilia Mkutano wa kawaida wa 23 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki uliokuwa ukiendelea jijini Arusha.

Mkutano huo pia ulihudhuria na Rais wa Shirikisho la Jamhuri ya Somalia Mhe. Hassan Sheikh Mahmoud ambaye alialikwa kuhudhuria mkutano huo.

Mkutano huu pia ulipokea na kuridhia kwa kauli moja mapendekezo ya Majadiliano ya Juu kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi na Usalama wa Chakula yaliyofanyika jijini Arusha tarehe 23 Novemba na kuhudhuriwa na Wakuu wa Nchi na Mawaziri wa Kisekta.

Kuridhiwa kwa mapendekezo hayo kunaifanya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwenda katika Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabia Nchi (COP28) utakaofanyika nchini UAE kuanzia tarehe 28 Novemba 2023 na msimamo mmoja wa nchi wanachama.

Mkutano huo ulijadili na kukubaliana juu ya masuala mbalimbali ya Mtangamano wa Afrika Mashariki ambapo wameazimia kuendelea kuulinda na kuukuza mtangamano huo kwa lengo la kuwaenzi waasisi wake na kuinua kipato cha watu na kutoa rai za kutokuruhusu tofauti ndogondogo kuleta mtafaruku ndani ya Jumuiya.

Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki wakiwa wamesimama wakati wimbo wa Afrika Mashariki unapigwa kwenye Mkutano wa 23 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akifuatilia Mkutano wa 23 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliokuwa ukiendelea katika viwanja vya Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.
Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki, Mhe. Stephen Byabato (Mb.) akifuatilia Mkutano wa 23 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliokuwa ukiendelea katika viwanja vya Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akifuatilia Mkutano wa 23 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliokuwa ukiendelea katika viwanja vya Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.

Rais wa Jamhuri ya Kenya Mhe. Dkt. William Ruto akizungumza kwenye Mkutano wa 23 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika katika Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.

Rais wa Somalia Mhe. Hassan Sheikh Mohamud akizungumza kwenye Mkutano wa 23 wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika katika Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha. Somalia imekuwa Mwanachama mpya wa Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya ombi lake la kujiunga na Jumuiya hiyo kuridhiwa kwenye mkutano.

Rais wa Burundi Mhe. Évariste Ndayishimiye akitoa hotuba ya ufunguzi kwenye Mkutano wa 23 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha.

Rais wa Uganda Mhe. Yoweri Museveni akihutuba ya ufunguzi kwenye Mkutano wa 23 wa Kawaida wa Wakuu wa Nchi Wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika katika viwanja vya Hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha





Idirisa Musa Hamadi kutoka Tanzania akipokea zawadi ya uandishi wa Insha


Viongozi hao wameitakia heri Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo katika uchaguzi mkuu unaotarajia kufanyika nchini humo.

Katika Mkutano huo Wanafunzi sita kutoka nchi wanachama walishinda tuzo ya uandishi wa Insha na kupatiwa vyeti na zawadi ya fedha taslimu. Wanafunzi walioshinda tuzo hizo ni Lalom Joselin kutoka Sudani Kusini aliyepata Dola 550 za Marekani, Ilimfuwe Aija kutoka Burundi alipata dola 600 za Marekani, Amoron Evelyn kutoka Uganda alipata Dola 770 za Marekani, Irasore sania kutoka Rwanda alipata Dola 1000, Idirisa Musa Hamadi kutoka Tanzania alipata Dola 1200 za Marekani na Austin Alego Angoya 1kutoka Kenya alipata Dola 1500 za Marekani.

Wanafunzi hao washindi wa Tuzo hizo pia wamepata zawadi ya kutembelea Hifadhi ya Taifa Tarangire, Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro na Hifadhi ya Taifa ya Mlima Kilimanjaro kuanzia tarehe 25 -27 Novemba, 2023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news