TANZIA: Mfanyakazi Upendo Media,Ruth Heslon afariki katika ajali

DAR ES SALAAM- Mfanyakazi wa Upendo Media Network Ltd (UMN) ni miongoni mwa abairia waliofariki katika ajali iliyohusisha basi la Kampuni ya Ally's na treni.
Hayo ni kwa mujibu w ataarifa iliyoonwa na chombo hiki kutoka kwa uongozi wa UMN ikifafanua kuwa, "Nasikitika kuwataarifu kuwa mtumishi mwenzetu wa Upendo Media, Ruth Heslon amefariki dunia alfajiri ya leo Novemba 29, 2023 kwa ajali ya basi iliyotokea huko Manyoni mkoani Singida.

"Ajali iliyosababisha kifo cha Ruth ilitokea baada ya basi la Ally's alilokuwa akisafiria kugonga kichwa cha treni.

"Marehemu alikuwa Afisa Masoko wa Upendo Media na alikuwa safarini kuelekea Karagwe kwenye harusi ya mdogo wake.Naomba tuungane na wanafamilia kuwaombea na kuwafariji katika kipindi hiki kiguma."Soma zaidi hapa kuhusu ajali hiyo>>>

BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LA BWANA LIHIMIDIWE

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news