Waziri Mkuu awataka Watanzania kushirikiana kutokomeza ukatili wa kijinsia

ZANZIBAR-Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ametoa wito kwa jamii ya watanzania kushirikiana na serikali na asasi za kiraia kupambana na matendo ya ukatili dhidi ya wanawake watoto na wenye ulemavu.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza wakati alipoongoza Mbio za Hisani za Kukomesha Ukatili wa Kijinsia (Top GBV Half Marathon ) 2023 zilizofanyika Mji Mkongwe Zanzibar, Novemba 26, 2023. Mbio hizo zimeandaliwa na Taasisi ya Asma Mwinyi ya Zanzibar. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

Amesema ili kupata matokeo ya haraka, wanajamii wahusishwe kuanzia hatua ya upangaji wa mikakati ambayo itatumika kutekeleza afua zinazohusu jamii yao.

"Namna hii itawawezesha kuzikubali afua hizo na kujiona kuwa ni sehemu muhimu katika utekelezaji. Wanajamii wasipangiwe bali washirikishwe kupanga mikakati inayohusu jamii zao."

Ameyasema hayo leo Jumapili Novemba 26, 2023 wakati alipomuwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika mbio za hisani za kutokomeza ukatili wa kijinsia dhidi ya wanawake, watoto na wenye ulemavu (STOP GENDER BASED VIOLENCE) zilizohitimishwa katika viwanja vya Forodhani mjini Zanzibar.

Aidha,Mheshimiwa Majaliwa, ameziagiza Idara na Mashirika ya Serikali yaimarishe ushirikiano na asasi za kiraia zinazotekeleza afua za kutokomeza ukatili wa kijinsia.

"Kwa kuwa Serikali zimeshaandaa mipango na mikakati ya kitaifa, asasi za kiraia zitekeleze shughuli zao kwa kuzingatia mipango hiyo ili kuharakisha utatuzi wa changamoto za kijinsia."

Mheshima Majaliwa amesema Serikali katika kutekeleza Sheria ya Msaada wa Kisheria Na. 1 ya mwaka 2017, imewezesha makundi maalum yakiwemo ya wanawake na watoto kupata haki zao katika vyombo vya usimamizi wa sheria.

"Serikali ya Mapinduzi Zanzibar imekuwa ikitoa msaada wa kisheria kwa waathirika wa matukio ya udhalilishaji wa kijinsia ambapo zaidi ya waathirika 1,700 wamepatiwa msaada wa kisheria na kisaikolijia katika mwaka 2022/2023."

Ameongeza kuwa, tayari Serikali imeunda madawati na vituo kwa ajili ya ulinzi na usalama wa Mmtoto na kutoa huduma za msingi kwa waathitika wa matukio ya ukatili wa kijinsia.

"Kwa upande wa Tanzania Bara; madawati 1,850 katika shule za msingi 1,128 na sekondari hadi kufikia Septemba, 2023. Kwa upande wa elimu ya kati na elimu ya juu madawati 273 yameanzishwa hadi kufikia Juni 2023."

Amesema kwa upande wa Zanzibar jumla ya madawati 40 yameundwa katika vituo vya Polisi ili kuharakisha utoaji huduma kwa waathirika wa ukatili wa kijinsia.Aidha vituo saba vya kutolea huduma za mahali pamoja vimeanzishwa Mnazi Mmoja, Makunduchi na Kivunge; Pia Wete, Mkoani, Chake Chake na Micheweni.

Aidha,Mheshimiwa Majaliwa Wizara, ameziagiza Idara na Mashirika ya Serikali yaimarishe ushirikiano na asasi za kiraia zinazotekeleza afua za kutokomeza ukatili wa kijinsia.

"Kwa kuwa Serikali zimeshaandaa mipango na mikakati ya kitaifa, asasi za kiraia zitekeleze shughuli zao kwa kuzingatia mipango hiyo ili kuharakisha utatuzi wa changamoto za kijinsia."

Kwa Upande, wake Waziri wa Vijana, Utamaduni na Michezo wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Tabia Maulid Mwita, amesema Serikali ya Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi imejizatiti katika kuhakikisha inadhibiti vitendo vya ukatili wa kijinsia.

Naye, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Asma Foundation, Asma Ali Mwinyi amesema mbio hizo za hisani zimelenga kukusanya shilingi Milioni 500 ambazo zitatumika kuwawezesha wanawake, watoto na wenye ulemavu waliopata changamoto za unyanyasaji wa kijinsia.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news