Ajali ya basi la Baraka yaua 14 mkoani Lindi

LINDI-Zaidi ya watu 14 wamefariki dunia katika ajali ya barabarani iliyohusisha basi la Kampuni ya Baraka Classic lenye namba za usajili T 336 DPW, linayofanya safari yake kutoka wilayani Tandahimba mkoani Mtwara kuelekea jijini Dar es Salaam.

Ajali hiyo imetokea leo Novemba 26, 2023 majira ya saa moja asubuhi katika eneo la Mtama na chanzo cha ajali hiyo kikielezwa kuwa ni breki za basi hilo kufeli.

Akithibitisha kutokea kwa ajali hiyo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi, John Imori amesema, miili ya marehemu imehifadhiwa katika Hospitali ya Nyangao pamoja na majeruhi 26 wanaendelea na matibabu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news