Yanga SC yawapiga Simba SC mabao 5-1 Derby ya Kariakoo

DAR ES SALAAM-Klabu ya Simba ya jijini Dar es Salaam imejikuta katika wakati mgumu kupitia Derby ya Kariakoo baada ya kupoteza kwa mabao 5-1.

Mtanange huo umepigwa leo Novemba 5, 2023 dhidi ya watani zao Yanga SC ya jijini Dar es Salaam katika Dimba la Benjamin Mkapa lililopo Halmashauri ya Manispaa ya Temeke jijini Dar es Salaam.

Kupitia Derby hiyo, kikosi cha Yanga kilipata bao la mapema dakika ya tatu kupitia kwa Kennedy Musonda kwa baada ya kumalizia mpira wa krosi uliopigwa na Yao Attohoula.

Aidha, Kibu Denis aliwapatia Simba SC bao la kusawazisha kwa kichwa dakika ya tisa akimalizia mpira wa kona uliopigwa na Said Ntibazonkiza.

Max Nzengeli aliwapatia Yanga bao la pili dakika ya 64 kwa shuti kali la chini chini baada ya kuwazidi ujanja walinzi wetu wa Kati.

Aziz Ki aliwapatia Yanga bao la tatu dakika ya 72 baada ya kupokea pasi safi kutoka kwa Clement Mzize.

Nzengeli aliwapatia Yanga bao la nne dakika ya 77 akiwa ndani ya 18 baada ya kupokea pasi safi ya Mzize. Bao la tano kwa klabu ya Yanga lilipelekwa nyavuni na Pacome dakika ya 87 kwa mkwaju wa penalti.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news