Zambia na Malawi zitajiunga na Umoja wa Ushoroba wa Kati-Profesa Kahyarara

PWANI-Katibu Mkuu Wizara ya Uchukuzi, Profesa Goius Kahyarara amesema,wizara yake inatarajia kuwa mwenyeji wa kikao cha mawaziri wa sekta ya miundombinu na usafirishaji kutoka katika nchi za umoja wa ushoroba wa kati akizitaja Tanzania, Uganda, Rwanda, Burundi na Jumuiya ya Demokrasia ya Kongo( DRC ), Mkutano huo unatarajia kufanyika jijini Dar es Salaam .

Kahyarara amesema zipo nchi zingine mbilli zilizowasilisha maombi ya kujiunga katika ushoroba huo ambazo ni Zambia na Malawi nakuwa maombi yao yatawasilishwa katika kikao hicho cha Mawaziri japo kwa upande wa makatibu wakuu wao wamekwisharidhia maombi hayo.

Amesema hayo leo Novemba 3, 2023 alipoitembelea bandari kavu ya Kwala iliyopo Mkoa wa Pwani,

Pia amesema kupitia Ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan iliyofanyika hivi karibu nchini Zambia kati ya mambo yaliyoafikiwa kwenye ziara hiyo ni pamoja na kuimarisha umoja wa ushoroba wa kati, reli ya Tazara na kuimarisha bandari ya Dar es Salaam.

Aidha amesema lengo kuu ni la ushoroba kuisaidia bandari ya Dar es Dalaam kupata mizigo mingi zaidi pamoja na kuhudumia nchi zinazoizunguka Tanzania hivyo juhudi za kuimarisha bandari ya Dar es salaam zinakwenda sambamba na kuimarisha bandari kavu ya Kwala iliyopo Bagamoyo.

"Bandari kavu ya kwala kwa sasa inatoa huduma zote za kibandari kama bandari zingine na kubwa zaidi itairahishia shughuli zianazoendele Bandari ya Dar Salaam hivyo mteja hatokuwa na haja ya kwenda ofisi za bandari zilizopo posta Jijini Dar es Salaam kwani wanaweza malizia michakato yao yote katika ofisi zilizopo bandari kavu ya Kwala,"amesema.

Kwa Upande wake Meneja Mmiliki Mamlaka ya Bandari Tanzania (TPA), Alexander Ndibalema amesema katika eneo la Bandari Kavu ya Kwala, Serikali imetenga maeneo kwaajili ya nchi zinazopata huduma katika Bandari ya Dar es Salaam akitaja nchi hizo kuwa ni Burundi, Rwanda, Malawi, Zimbabwe, Uganda na Sudan Kusini ambazo zimetengewa hekta 10 kila mmoja na hekta 20 kwa nchi ya Zambia na Jamhuri ya Demokrasia ya Congo (DRC).

Ndibalema ameongeza kuwa bandari ya Kwala imeunganishwa na mtandao wa reli ya MGR ambao ndio unaosafirisha makasha kati ya Bandari ya Dar es Salaam na bandari hiyo na kwamba mipango ya Serikali iliyopo sasa nikuiunganisha pia bandari hiyo na mtandao wa reli ya SGR .

Amebainisha kuwa kwa sasa bandari hiyo inaweza kubeba makasha 3500 kwa wakati mmoja na ina uwezo wa kuhudumia makasha 300,000 kwa mwaka, hivyo itakuwa imesaidia kupunguza msongamano katika Bandari ya Dar es Salaam kwa takribani asilimia 30 ya shehena zinazoshushwa.

Kwa upande wake Kaimu Mkurugenzi Mwendeshaji, Focus Makoye amesema baada ya serikali kutoa maelekezo kujengwa bandari hiyo katika awamu ya kwanza, Shrika la Reli Tanzania liliweka jitihada kuunganisha miundombinu ya reli yenye kilomita 89 kutokea Dar es Salaam pamoja na kuweka njia tano za reli ambazo zina uwezo wa kuweka mabehewa 100 kwa wakati mmoja ambapo njia moja hubeba mabehewa 20.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news