Balozi wa India nchini amuaga Rais Dkt.Mwinyi,ashukuru

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi amekutana na Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe.Binaya Srikanta Pradhan Ikulu jijini Zanzibar kumuaga.
Mheshimiwa Balozi Binaya amefika Ikulu tarehe 22,2023 baada ya kumaliza kipindi cha miaka mitatu ya utumishi nchini.

Rais Dkt.Mwinyi amemshukuru kwa kudumisha ushirikiano na uhusiano wa kidiplomasia katika kipindi chake cha uwakilishi ikiwemo upatikanaji wa fursa mbalimbali za ufadhili wa masomo India.

Pia, kuanzishwa kwa Taasisi ya IIT Madras Zanzibar, miradi mbalimbali ya maendeleo, kujenga uwezo, pamoja na fursa za uwekezaji na biashara.

Naye , Balozi Mhe.Binaya Srikanta Pradhan amezungumzia kuhusu Serikali ya India kuwapeleka kikundi cha Zanzibar One Modern Taarab kutoka Zanzibar kushiriki Tamasha la Utamaduni nchini India mwezi Februari mwaka 2024.

Pia Balozi Mhe.Pradhan amemwalika Rais Dkt.Mwinyi kuitembelea India.Rais Dkt.Mwinyi amekubali mwaliko huo wa kuitembelea India.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news