Diaspora wahamasishwa kuwekeza hapa nchini

KAGERA-Waziri wa Ujenzi na Mbunge wa Jimbo la Karagwe, Innocent Bashungwa ametoa wito kwa wazawa wa Kagera wanaoishi nje ya mkoa pamoja na nje ya nchi Diaspora kuja kuwekeza mkoani humo kwani Serikali imeshaweka mazingira wezeshi na rafiki ya uwekezaji.
Ametoa wito huo leo Desemba 25, 2023 katika ibada ya Krismasi katika Parokia ya Bikira Maria Mbarikiwa Bushangaro - Nyakaiga, Karagwe mkoani Kagera iliyoongozwa na Paroko wa Parokia hiyo Padri Edward Rwechungura pamoja na Padri Georges Kimonges.

"Diaspora pamoja na majukumu ambayo Mwenyezi Mungu ametujalia kuwa katika maeneo mbalimbali ya nchi na mikoani lakini tusisahau kuwekeza nyumbani na niwapongeze Wanakagera wanaoendelea kuwekeza katika mkoa wetu,”amesema Bashungwa.
Waziri Bashungwa amesema Serikali inayoongozwa na Mheshimiwa Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan inaendelea kuboresha miundombinu ya barabara nchini ikiwemo mkoa Kagera ambao unaendelea kuunganishwa na nchi jirani kwa ujenzi wa barabara za lami.
"Kwa mfano kwetu sisi ukanda wa Bushangaro, mawasiliano ya barabara hayakuwa mazuri lakini barabara zinazidi kuboreshwa na 'Diaspora' mnapokuja mmekuwa mkinipigia kunieleza mambo yalivyobadilika,”amesema Bashungwa.
Aidha, Waziri Bashungwa ametoa wito kwa Wananchi wa mkoa wa Kagera kuendelea kumuunga mkono na kumuombea afya njema, Mheshimiwa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassn ili azidi kutenda kazi yake ya kuletea maendeleo ambapo amesema kazi ya kuwahudumia wananchi ni ngumu hivyo inahitaji maombi ambayo yatamlinda na kumsaidia kuzidi kuwa na hekima na busara katika uongozi wake.
Katika mahubiri, Padri Georges Kimonge amekemea tabia ya vijana kujihusisha na matendo yasiyompendeza Mungu hususan suala la kutoa Mimba ambapo amesema si jambo zuri kuua kiumbe ambacho Mwenyezi Mungu amepanga kukileta duniani kwa sababu maalum.
"Unapotoa mimba unamtoa Rais, unamtoa Waziri Mkuu, unamtoa Mfalme lakini vile vile silaumu akina mama wanaotoa mimba lakini akina Baba ndio mnaowapa hizo mimba akija akikwambia nina mimba unatumia lugha anasema nina mzigo kwa hiyo mama akienda kutoa mimba anaona ametoa mzigo,"amesema Padri Kimonge.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news