Tusherehekee Sikukuu ya Krismasi kwa furaha, amani na upendo-Prof.Muhongo

NA FRESHA KINASA

MBUNGE wa Jimbo la Musoma Vijijini Mkoani Mara Prof. Sospeter Muhongo amewatakia heri Wananchi wa Jimbo la Musoma Vijijini na Watanzania wote wanaposherehekea Sikuu ya Krismasi.
Ambayo Prof. Muhongo ameshauri kusherehekea kwa furaha, amani, upendo na kumtegemea Mungu katika mipango mbalimbali hasa mwaka mpya wa 2024 kwa kila mmoja na jamii kwa ujumla.

Prof. Muhongo amesema kuwa,"Krismasi 2023, Tusherehekee Sikukuu hii tukiwa na furaha, upendo na amani tele. Mungu yu pamoja nasi sote," amesema na kuongeza kuwa,

"Mwaka mpya 2024 Uwe mwaka wenye mafanikio makubwa kwa kila mmoja wetu na kwa jamii yote. Tuliyoyapanga, tuyatekeleze kwa ufanisi na ubora wa hali ya juu. Hakuna kushindwa," amesema Prof. Muhongo.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news