Familia ya Nabii Mkuu Dkt.GeorDavie yathibitisha kifo cha kijana wao Nic Davie (Director Nisher)

ARUSHA-Director maarufu wa video mbalimbali ikiwemo za wasanii wa Bongofleva ambaye pia ni Mtoto wa kwanza wa muhubiri maarufu wa Arusha wa Kanisa la Ngurumo ya Upako, Dkt.GeorDavie, Nic Davie maarufu Nisher amefariki saa nane na dakika tisa usiku wa kuamkia leo Desemba 12,2023.
Familia ya Dr.GeorDavie imethibitisha kutokea kwa msiba huo wa Kijana wao Nisher na kusema msiba unafanyika katika nyumba ya matamko Kisongo jijini Arusha na kwamba taarifa zaidi zitatolewa baadaye.

"FAMILIA YA NABII MKUU.MHE.DKT.GEORDAVIE INASIKITIKA KUTANGAZA KIFO CHA KIJANA WAO MPENDWA NIC DAVIE (NISHER) KILICHOTOKEA USIKU WA KUAMKIA LEO SAA NANE NA DAKIKA TISA.

"MSIBA UNAFANYIKIA KATIKA NYUMBA YA MATAMKO KISONGO ARUSHA TANZANIA!! 2TIMOTHEO4:7."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news