Hakuna mwananchi aliyefukuzwa Loliondo-Serikali

DODOMA-Serikali imesema kuwa hakuna mwananchi yoyote anayefukuzwa katika eneo la Loliondo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 2,500 ambalo lilimegwa kutoka pori la akiba Pololeti katika Wilaya ya Ngorongoro ambalo Serikali ililitoa kwa ajili ya shughuli za wananchi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dodoma, Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari-Maelezo, Bw.Mobhare Matinyi amesema taarifa hizo hazina ukweli wowote, kwani Serikali ilikabidhi eneo hilo kwa ajili ya matumizi ya Wananchi kufuatia kumegwa kwa lililokuwa pori tengefu la Loliondo mwaka 2022.

Amebainisha kuwa, awali pori hilo lilikuwa na ukubwa wa kilomita za mraba 4,000 ambapo baada ya kugawanywa Kilomita za mraba 1,500 ambazo ndio Pori la Akiba Pololeti zilibaki kwa ajili ya shughuli za uhifadhi na Kilomita za Mraba 2,500 Serikali ilizitoa kwa ajili ya Wananchi kufanya shughuli zao za maendeleo.

Bw.Matinyi alisisitiza kuwa serikali itaendelea kusimamia shughuli za uhifadhi katika eneo la Ngorongoro na kuwataka wananchi kupuuza taarifa hizo kwa kuwa Serikali inatekeleza majukumu yake kwa kuzingatia sheria, kanuni, taratibu na kufuata misingi ya haki za binadamu.

Amewataka wananchi wote wanaoishi katika eneo walilopewa na Serikali lenye kilomita za mraba 2500 kuendelea na shughuli zao na kupuuza taarifa hizo zenye lengo la kupotosha umma.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news