MAAFA KATESH:Dkt.Yonazi aipongeza Muhimbili

MANYARA-Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge na Uratibu) Dkt. Jim Yonazi ameipongeza Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa kupeleka msaada wa dawa, vifaa tiba pamoja na Msaikolojia Tiba kwa wananchi wa Mji mdogo wa Katesh wilayani Hanang', mkoani Manyara ili kusaidia jitihada za utoaji huduma.
Eneo hilo lilikumbwa na maafa ya mafuriko yaliyosababisha maporomoko ya udongo kutoka mlima Hanang' na kuleta madhara makubwa ikiwemo vifo, majeruhi, upotevu wa mali na uharibifu wa miundombinu.

Dkt. Yonazi amesema, MNH imepeleka mchango ambao una aina mbalimbali (varieties) na kuwataka wengine kuiga mfano huo.

Akikabidhi dawa na vifaa tiba, Msaikolojia Tiba kutoka MNH, Bi. Egla Fugusa amesema, msaada huo una thamani ya shilingi milioni 38.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news