MAAFA KATESH:Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) yatoa pole

Kuhusu TEA

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) ilianzishwa kwa Sheria ya Mfuko wa Elimu Na.8 ya mwaka 2001 ikiwa na jukumu la kusimamia Mfuko wa Elimu wa Taifa. Sheria hiyo ilifanyiwa marekebisho mwaka 2013.

Madhumuni ya Mfuko wa Elimu ni kuongeza nguvu za Serikali katika kugharimia miradi ya elimu ili kuinua ubora wa elimu na upatikanaji wake kwa usawa, katika ngazi zote za Elimu kwa Tanzania Bara na Elimu ya Juu kwa Tanzania Zanzibar.

Kuanzia mwezi Oktoba 2017, Mamlaka pia ilipewa jukumu na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia la kusimamia na kuratibu Mfuko wa Kuendeleza Ujuzi (Skills Development Fund (SDF)).

Mfuko huu ni sehemu ya Programu ya Kuendeleza Elimu ya Ujuzi na Mafunzo ya Stadi za Kazi zenye kuleta tija katika ajira (Education and Skills for Productive Jobs (ESPJ) na Mpango Mkakati wa Kitaifa wa Kukuza na Kuendeleza Ujuzi (National Skills Development Strategy (NSDS).

Mfuko wa SDF ulikuwa unatoa ufadhili wa mafunzo ya kuendeleza ujuzi katika sekta sita za kipaumbele zinazoratibiwa na Programu ya ESPJ, ambazo ni Kilimo na Kilimo Uchumi, Utalii na huduma za ukarimu,Uchukuzi, Ujenzi, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) na Nishati.

Ufadhili na utekelezaji wa miradi ya Kuendeleza Ujuzi awamu ya kwanza ya ESPJ ulikuwa wa miaka mitano,kuanzia mwaka 2018/2019 ambao ulikamilika mwezi Juni 2023.

Mamlaka inaongozwa na Bodi yenye Wajumbe wanaoteuliwa na Mhe. Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia. Mwenyekiti wa Bodi huteuliwa na Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Mkurugenzi Mkuu ni Katibu wa Bodi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news