MAAFA KATESH: Kundi la WhatsApp la Hanang' Yetu Forum watoa katoni 182 za maji

NA DIRAMAKINI

KUNDI Sogosi la Hanang' Yetu Forum la WhatsApp limekabidhi kwa Kamati ya Maafa Mkoa wa Manyara katoni 182 za maji kwa ajili ya kusaidia waathirika wa mafuriko yaliyotokana na maporomoko huko Katesh.

Janga hilo lilitokea Desemba 3, 2023 kwenye mji mdogo wa Katesh na vitongoji vya karibu vya Jorodom, Ganana, Katesh na Dumbeta pamoja na vijiji vya Gendabi, Sarijandu, Arukushay na Sebasi, wilayani Hanangi mkoani Manyara.

Aidha, maafa hayo yalifuatia mvua kubwa iliyonyesha usiku Jumamosi, tarehe 02 Desemba, 2023 na hatimaye kufuatiwa na tukio hilo alfajiri ya Jumapili, tarehe 3 Desemba, 2023 majira ya saa 11:30.

Kwa niaba ya wanakikundi hicho, Jabischi Bwanjida Langay (JB) amekabidhi msaada huo kwa Kamati ya Maafa Mkoa wa Manyara ambao ulitokana na wanakikundi kuchangia shilingi 819,000 ili kuungana na Watanzania ambao wanaendelea kuchangia kwa ajili ya kuwasaidia waathirika hao.

Vile vile,Serikali imetoa wito kwa kampuni, mashirika, taasisi za umma na binafsi, wadau mbalimbali na wananchi kwa ujumla kujitolea kwa hali na mali ili kuwaisaidia wenzetu waliopatwa na janga hili. Bado kuna uhitaji wa vyakula, vifaa, mitambo,madawa na mahitaji mengine.

Kwa misaada ya fedha, Waziri Mkuu ameelekeza, kwamba mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Maafa Na. 6 ya mwaka 2022 na kanuni zake za mwaka 2022, fedha zote zitumwe kwenye akaunti ya Kamati ya Maafa ya Taifa:

National Disaster Management Fund Electronic Account 9921151001 kwa kuandika neno MAAFA HANANG. Benki yoyote ndani na nje ya nchi inaweza kupokea fedha kupitia akaunti hii.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news