MAAFA KATESH:Muhimbili yapeleka Msaikolojia, dawa na vifaa tiba

DAR ES SALAAM-Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imeungana na wananchi wa Mji mdogo wa Katesh Wilayani Hanang, Mkoani Manyara na kupeleka msaada wa dawa na vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 38 ili kusaidia jitihada za utoaji huduma katika eneo hilo.
Ni eneo ambalo hivi karibuni lilikumbwa na maafa ya mafuriko yaliyosababisha maporomoko ya udongo kutoka mlima Katesh na kuleta madhara makubwa ikiwemo vifo, majeruhi, upotevu wa mali na uharibifu wa miundombinu.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa MNH, Mkuu wa Idara ya Famasi, Mfamasia. Nelson Faustine amesema sambamba na msaada huo, Hospitali imetuma Msaikolojia Tiba kwenda kuungana na timu za watalam mbalimbali walioko kule wanaotoa huduma kwa waathirika wa mafuriko hayo.
Hatua hii pia ni kuitikia wito wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan ambaye ameagiza kupelekea watalaam wa saikolojia kuzungumza na wananchi waliopata mfadhaiko kutokana na tukio hilo ili waweze kurejea katika hali ya kawaida.
Bodi ya Wadhamini, Menejimenti na Wafanyakazi wa Hospitali ya Taifa Muhimbili wanaendelea kutoa pole kwa wananchi wa Mji mdogo wa Katesh Wilayani Hanang, Mkoani Manyara kutokana na madhara waliyopata.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news