MAAFA KATESH:Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar atoa pole,akabidhi msaada

MANYARA-Spika wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar,Mhe. Zubeir Maulid ameipongeza kazi kubwa iliyofanywa na Serikali na Wananchi waliojitolea kusaidia Waathirika wa maafa ya maporomoko ya mawe na tope kutoka Mlima Hanang’ mkoani Manyara.
Ametoa kauli hiyo alipoongoza ujumbe kutoka Baraza la Wawakilishi kutoa msaada wa kibinadamu kwa waathirika wa maporomoko hayo katika Halmashauri ya Wilaya ya Hanang' yaliyotokea Desemba 3, 2023.
Alieleza kwamba, jambo hili limeonesha kiasi gani nchi yetu ina umoja hususani tunapopata matatizo na namna gani tunashirikiana kama ndugu kulitatua.

"Tumekuja tumeleta kiasi cha shilingi milioni 30 tunajua mahitaji ni makubwa, lakini kidogo kidogo, tukiunganisha nguvu zetu jambo litakuwa kubwa ili isaidie waathirika, “alibainisha.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera Bunge na Uratibu, Mhe. Jenista Mhagama amewashukuru, baraza la wawakilishi kwa msaada wa kibinadamu walioutoa kwa waathirika.

“Jambo hili limeonesha kwamba Muungano wetu si Muungano wa maneno bali ni Muungano wa vitendo,” alifafanua Waziri Mhagama.
Aliongezea kuwa, Serikali itaendelea kuratibu vyema suala hilo na kuhakikisha kila mchango unatumika kwa lengo lililokusudiwa na si vinginevyo na kuongezea kwamba watadhibiti kila mianya ya ubadhilifu na kusisitiza kuwa kwa yeyote atakayefuja michango hiyo hatua za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news