Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu:Barabara ya Jumbi Sokoni Kibondeni hadi Hospitali yazinduliwa

ZANZIBAR-Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za Serikali ya Mapinduzi Zanzibar (SMZ), Mhe. Masoud Ali Muhammed amewataka wananchi kuzilinda na kuzitunza Barabara walizojengewa ili ziendelee kudumu kwa muda mrefu.

Wito huo ameutoa huko Kibondeni katika uzinduzi wa Barabara ya Jumbi Sokoni Kibondeni hadi Hospitali yenye Kilomita 4.4 ikiwa ni miongoni mwa Maadhimisho ya Miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Amesema, Serikali inatumia pesa nyingi kwa ajili ya kuwapatia wananchi maendeleo hivyo iko haja ya jamii kuilinda kuitunza miundombinu hiyo sambamba na kutoa Elimu kwa wale wote wanaovamia hifadhi ya barabara.

"Ni wajibu wetu kuhakikusha Barabara zetu hizi tunazitunza kwa kulinda miundombinu iliyowekwa," alisisitiza Waziri.

Aidha, amezikumbusha mamlaka zinazotoa vibali vya ujenzi kuhakikisha wanasimamia kwa kuzingatia miundombinu ya Barabara ili kuzilinda na kuepusha ajali.

Amefahamisha kuwa uzinduzi wa Barabara hiyo ni miongoni mwa ahadi za Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi katika kuimarisha miundombinu ya kujenga Barabara kuu na za ndani kwa kiwango cha lami kwa Unguja na Pemba.

Ameongeza kuwa, kukamilika kwa barabara hiyo kutawarahisishia wananchi katika shughuli zao za kiuchumi na kujipatia kipato.
Aidha, amesema maendeleo yaliyoletwa na Hayati Karume yamekuwa yakiendelezwa kwa awamu zote za uongozi katika awamu ya nane miradi mbalimbali ya maendeleo imetekelezwa ikiwemo barabara za kiwango cha lami,majengo ya skuli za ghorofa, hospitali kwa kila wilaya, masoko na mengineyo.

"Lengo la Mapinduzi ni kutekeleza yale yaliyoletwa na hayati Karume ili kuhakikisha zinaendelezwa kwa uhakika,”alifahamisha Waziri.

Akitoa taarifa ya kitaalamu Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi, Mhandisi Shomari Omar Shomari amesema zaidi ya dola za kimarekeni milioni moja zimetumika katika ujenzi huo.

Amefahamisha kuwa, barabara hiyo ni miongoni mwa barabara za ndani zinazojengwa na Kampuni ya Airis kutoka Uturuki zenye uwezo wa kupita gari zenye uzito wa tani 10.

Ufunguzi wa barabara ya kilomita 4.4 in shamrashamra za kuelekea kutimiza miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news