Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu:Hoteli ya kifahari ya SBH Monica Zanzibar yafunguliwa

ZANZIBAR-Waziri Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe. Lela Muhamed Mussa amezitaka Wizara zinazohusika na Uwekezaji kusimamia usalama wa wageni ili kuondosha hofu katika miradi yao.

Wito huo ameutoa huko Paje katika ufunguzi wa Hoteli ya SBH Monica, yenye hadhi ya nyota tano ikiwa ni shamrshamra za kutimiza miaka 60 ya Mapinduzi.

Amesema, Serikali inaendelea kuweka mazingira bora kwa wawekezaji na wageni ili kuwaondoshea hofu na usumbufu unaoweza kujitokeza.

Aidha, amesema ufunguzi wa hoteli hiyo utaongeza idadi ya ajira na kunyanyua uchumi wa nchi.

Amesema, mafanikio hayo yaliopatikana yanatokana na kuwepo kwa amani na utulivu hivyo ni vyema kuiunga mkono Serikali katika kufanikisha malengo yake.

"Ogezeko kubwa la wawekezaji linatokana na amani na utulivu ulilopo nchini kwetu hivyo tuendelee kuyatunza mapinduzi yetu kwa maslahi yetu,"alifafanua Waziri Lela

Aidha, ameeleza kuwa Zanzibar inasifika kwa vitu vya asili hivyo hakuna budi kuviweka vitu hivyo katika hoteli zao ili kuvutia wageni wanaoingia nchini.

Akitoa Maelezo ya kitaalamu Mkurugenzi Mtendaji wa Mamlaka ya Uwekezaji (ZIPA) Sharif Ali Sharif amesema, hoteli hiyo ina vyumba mia moja na ina uwezo wa kutoa huduma kwa wageni 109 kwa wakati mmoja.

Ameongeza kuwa, katika hoteli hiyo tayari wameshaajiri vijana zaidi ya 90 na wanatarajia kuajiri wengine 68 ili kuinua kipato cha Wananchi.

NaYe Katibu Mkuu wa Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais, Kazi, Uchumi na Uwekezaji Habiba Hassan amesema Serikali ya awamu ya nane inakwenda kwa kasi ya kuweka kipaumbele maeneo ya Uwekezaji.

Amefahamisha kuwa, Serikali imefanya marekebisho ya Sheria ya uwekezaji ili wawekezaji waweze kujisajili na kuongeza pato la Taifa.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news