Miaka 60 ya Mapinduzi Matukufu:Soko la Mazao ya Baharini Kikungwi lafunguliwa

ZANZIBAR-Waziri wa Afya Zanzibar,Nassor Ahmed Mazrui amewataka wajasiriamali wa Soko la Chaza Kikungwi kudumisha usafi ili liwe endelevu na kivutio kwa watalii.

Akizungumza katika uzinduzi wa soko la mazao ya baharini, huko Kikungwi Wilaya ya Kati, ikiwa ni shamrashamra ya miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar amesema, watalii wanaoingia nchini wanapenda mazao ya Baarini ikiwemo Chaza hivyo ni vyema kudumisha usafi katika maeneo yao.

"Usafi ni muhimu na biashara ya Chaza inapendwa na wageni wa kitalii,”alisema Waziri huku akiwataka kufuata utaratibu wa wafanyabiashara wa chakula kwa kupima afya zao na kuvaa nguo maluum zinazotakiwa.

Akisoma taarifa ya kitaalamu, Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Idara Malum za SMZ, Issa Mahfoudhi Haji alisema ujenzi wa soko hilo itapelekea kuondoa changamoto zinazowakabili wafanyabiashara hao.

Naye Katibu wa Kikundi cha kuuza Chaza Kikungwi, Bahati Issa Suleiman alisema kuwepo kwa soko hilo kumewapa faraja kwani ni soko la uhakika la kuuzia bidhaa zao sambamba na kuahidi kulienzi na kulitunza ili liweze kuwa endelevu.

Soko hilo limejengwa na kampuni ya Mzawa Modarn Building Contractor LTD, umegharimu zaidi ya milioni 300 ambapo ujenzi wake ulianza Machi 23,2023 na umekamilika rasmi Novemba 25,023.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news