Rais Dkt.Mwinyi ashukuru

ZANZIBAR-Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi amekutana na Naibu Mkurugenzi Mkuu Umoja wa Ulaya nchini Tanzania, Martin Seychell na ujumbe wake Ikulu Zanzibar tarehe 7 Desemba 2023.
Katika mazungumzo yao wamegusia uhusiano uliopo kati ya Zanzibar na Umoja wa Ulaya katika kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo Elimu, Nishati, Afya, Maji na miundombinu nchini.

Pia sekta ya Utalii, Uchumi wa Buluu hususani Uvuvi na Kilimo cha Mwani.

Kwa upande mwingine Rais Dkt. Mwinyi amewashukuru Uongozi wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Ushirikiano wa Elimu Duniani (GPE) kwa kufanyia vikao vyao Zanzibar ikiwa ni mara ya kwanza kufanyika nje ya Bara la Ulaya na Amerika pamoja na kuisadia Zanzibar hususani katika sekta ya elimu.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news