Serikali yajipanga kuongeza virutubisho vya vitamini na madini kwenye vyakula

DODOMA-Serikali imejipanga kuongeza virutubisho vya vitamini na madini kwenye vyakula ambavyo vitasadia kuimarisha kinga ya mwili ikiwa ni jitihada za kuhakikisha changamoto ya ukosefu wa lishe yanayowakabili Watanzania hususani wakinamama wajawazito ambao upelekea kuzaa watoto wa vichwa vikubwa na mgongo wazi inatoweka.
Kauli hiyo imetolewa Desemba 14,2023 jijini Dodoma na Mtafiti na Mratibu wa shughuli za uongezaji virutubishi kitaifa, Selestine Mgoba wakati alipokuwa kwenye warsha ya utiaji maoni kanuni za kuongeza virutubisho kwenye vyakula iliyoandaliwa na Wizara ya Viwanda na Biashara na kuwakutanisha wanakamati kutoka Wizara mbalimbali na Sekta binafsi.
"Tunaona kwenye Taifa letu upungufu wa Damu ambao unasababishwa na upungufu wa madini chumvi, zaidi ya asilimia 59 ya watoto wa kitanzania chini ya umri wa miaka mitano wana upungufu wa Damu, kwa hiyo wazalishaji vyakula wakiwa na utaratibu wa kuongeza madini chumvi kwenye vyakula tulivyo vibainisha ikiwemo unga wa ngano, unga wa mahindi,mafuta ya kula na chumvi itasaidia," amesema Mtafiti Mgoba.
Aidha, Mgoba amesema katika kuboresha lishe nchini kuna kiwanda ambacho kinaanzishwa ili kurahisisha upatikanaji wa virutubisho kwa wakati tofauti na hapo awali ambavyo ilitakiwa kuagiza nje ya nchi.
Naye Kaimu Mkurugenzi Idara ya Viwanda Vidogo na Biashara ndogo wa Wizara ya Viwanda na Biashara Mhandisi Ilege Charles amesema kuwa wazalishaji wengi wa vyakula ni wadogo ambao jukumu kubwa la Wizara kupitia Shirika la Viwango Tanzania kwa kushirikiana na Halmashauri ni kuwasimamia na kuwapa elimu ya jinsi ya kuchakata na kuzalisha vyakula vyenye virutubisho ili kuondoa changamoto ya watoto wanaozaliwa na migongo wazi na vichwa vikubwa.
Kwa upande wake Afisa Lishe Mwandamizi Peter Kaja kutoka Wizara ya Afya amesema Takwimu za mwaka 2022 zinaonesha hali ya udumavu nchini imefika asilimia 30 kutoka asilimia 31 licha ya kwamba ipo baadhi ya mikoa ipo mpaka asilimia 56 na lengo la nchi ni kufikia asilimia 20 ya udumavu na wakina mama wakitumia madini chuma itasaidia kupambana na tatizo hilo wakati wa kujifungua.
Naye Tumsime Nkyando Mkurugenzi Mkaazi wa Shirika la Kimataifa lisilo la Kiserikali la TechnoServe amesema Kanuni zinazojadiliwa zitaleta tija kubwa katika kujenga afya njema kwani watu wasipokuwa na lishe inaweza kupelekea kutokuwa na uwezo mkubwa wa kimaamuzi na kufikiria zaidi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news