Serikali yatumia taarifa za Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi kutambua waathirika Hanang'

RUVUMA-Serikali imetumia taarifa za matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika mwaka 2022 kuthibitisha taarifa za makazi na kaya katika maeneo yaliyoathirika na mafuriko ya matope wilayani Hanang'.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu) Mhe. Jenista Mhagama akipokea Kitabu cha Sensa ya watu na makazi Kutoka kwa Bw.Seif Kuchengo, Mratibu wa Sensa Taifa (Katikati) na upande wa kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Ruvuma,Odo Mwisho wakati wa ufunguzi wa Mafunzo ya Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 kutoka kwa Viongozi na Watendaji wa Mkoa wa Ruvuma, Kamati za Sensa na Wawakilishi wa Makundi Mbalimbali katika jamii.

Kauli hiyo ameitoa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu),Mhe. Jenista Mhagama wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya matumizi ya matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022 kwa Viongozi na Watendaji wa Mkoa wa Ruvuma, iliyohusisha Kamati za Sensa na Wawakilishi wa Makundi Mbalimbali katika jamii.

Ni Desemba 23,2023 katika ukumbi wa Njunde Social Hall – Halmashauri ya Wilaya ya Songea mkoani Ruvuma.
Waziri alisema, moja ya jukumu muhimu walilokuwa nalo ni kupata taarifa ya hali ya kaya, makazi na mali katika maeneo yaliyoathirika kabla ya maafa hayo.

“Hitaji hili lilipelekea timu ya wataalamu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu kuja na taarifa ya kitaalamu iliyoambatana na picha za satelite ambazo zilionesha kwa uhakika hali ya kaya, makazi na mali zilizokuwepo katika maeneo hayo kwa idadi yake na maeneo zilizokuwepo.,” alibainisha.
Aliongeza kuwa,licha ya kwamba wametumia vyanzo vingine pia kuthibitisha baadhi ya masuala katika maeneo hayo, lakini chanzo chao cha kwanza cha kuaminika kimekuwa ni Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022.

Aidha,alitumia fursa hiyo kuwakumbusha kuhusu maandalizi ya Dira ya Taifa 2050 ambapo serikali imetoa fursa kwa wananchi kutoa maoni na mapendekezo.

”Niwasihi sana viongozi, watendaji na wananchi wote mshiriki katika zoezi hili ambalo ni muhimu kwa mustakabali mwema wa maendeleo ya nchi yetu.
"Moja ya nyenzo muhimu zinazoweza kutuongoza kutoa maoni yetu ipasavyo historia ya taifa letu katika nyanja zote za siasa, uchumu, jamii pamoja na kuzingatia takwimu zinazozalishwa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu ikiwemo ya matokeo ya sensa ya watu na makazi ya mwaka 2022,”alifafanua.

Kwa upande wake Mwantumu Athumani, Meneja Takwimu Mkoa wa Ruvuma akizungumza kwa niaba ya Mtwakwimu Mkuu wa Serikali, alisema utoaji wa matokeo ya sensa ni tofauti na matukio mengine ya kitakwimu kwa kuwa wigo wa sensa ni mpana zaidi.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera Bunge na Uratibu),Mhe. Jenista Mhagama akimkabidhi ramani Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea, Bi, Neema Maghembe wakati Mafunzo ya Matumizi ya Matokeo ya Sensa ya Watu na Makazi.

”Matokeo ya sensa hutolewa awamu kwa awamu kulingana na ratiba ya utoaji na usambazaji wa matokeo,” alisema.

Ameongeza kuwa, kama kuna mdau anahitaji matokeo ya sensa, ambayo hayapo kwenye ripoti zao kwa sasa anakaribishwa kuleta maombi yake kwenye ofisi za mikoa.

Naye Mkazi wa Peramiho, Bw. Tito Sowela alisema elimu ya sensa ya watu na makazi imeongeza uelewa mpana wa wananchi hasa juu ya taarifa zinazokusanywa na namna zinavyoweza kusaidia serikali katika kupanga miradi ya maendeleo kwa wananchi.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news