Tujifunze kwa Mama Bikira Maria-Padri Masanja

NA ADELADIUS MAKWEGA

WAKRISTO wameambiwa kuwa, yako mengi ya kujifunza kutoka kwa Mama Bikira Maria katika Dominika ya Nne ya Majilio,kwani japokuwa aliambiwa jambo la utatanishi mkubwa alilipokea na kulikubali, kama yalivyo mapenzi ya Mungu.
Hayo yamesemwa na Padri Samson Masanja, Katika Kanisa la Bikira Maria–Malkia wa Wamisionari Parokia ya Malya, Jimbo Kuu Katoliki la Mwanza, katika misa ya kwanza ya dominika ya nne ya Majilio leo Disemba 24, 2023.

“Kukubali kwake mpango wa mwenyezi Mungu ni ishara ya unyenyekevu, ni ishara ya unyofu wa moyo na ni ishara ya kujishushwa kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu.”

Padri Masanja aliongeza kuwa, agizo hilo la Malaika Gabrieli kutoka kwa Mungu hata kama lingemfikia mtu wa leo lingekuwa jambo gumu na pengine hali ingekuwa tofauti zaidi.

Padri Masanja alisema kuwa,kwake Mungu hakuna kinachoshindikana, hata mambo yote yawe magumu namna gani yanakamilika.

Misa hiyyo pia iliambatana na nia na maombi kadhaa,“Utasaidie kuzikipokea kazi na wajibu ambazo umetukabidhi tuzitimize , ee Bwana - Twakuomba utusikie.”

Hadi misa hiyo inamalizika majira ya saa moja ya asubuhi, hali ya hewa ya Malya na viunga vyake ni mvua na jua, sasa wakulima wakipandikiza mipunga yao kwa mabonde kwa juhudi kubwa kutoka vitaluni.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news