TANZIA:Mwanahabari wa DW Kiswahili,Ahmad Juma Abdallah afariki jijini Dar es Salaam

BORN-Mwanahabari wa Idhaa ya Kiswahili ya Ujerumani (DW),Bw.Ahmad Juma Abdallah amefariki.
Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa hivi punde kupitia ukurasa rasmi wa DW Kiswahili kupitia mtandao wa Facebook.

"Tunasikitika kutangaza kifo cha mwenzetu Ahmad Juma Abdallah kilichotokea leo saa sita mchana katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili nchini Tanzania.

"Ahmad alikuwa amejikita zaidi kwenye vidio na makala za redio. Tunatoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki zake kutokana na msiba huo. Sote ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake turarejea,"imefafanua sehemu ya taarifa hiyo ya DW Kiswahili.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news