TASAC yachukua hatua kutokana na Meli ya MV. Wankyo kuigonga Meli ya MV.Kyone jijini Mwanza

DAR ES SALAAM-Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) limesema limeona taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu tukio la Meli ya MV. Wankyo kuigonga Meli ya MV. Kyone.

Ni tukio lililotokea Desemba 8, 2023 majira ya 10:25 jioni jijini Mwanza wakati ikitokea Bandari ya Bukoba kuelekea bandari ndogo ya Igogo iliyoko Mwanza Kusini (Mwanza South).

Hayo ni kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Desemba 17,2023 na Ofisi ya Mkurugenzi Mkuu,Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC).
Kufuatia taarifa hizo, TASAC imesema imefanya uchuguzi wa awali ambapo imethibitisha kutokea kwa tukio hilo na tayari hatua za awali za kisheria zimeanza kuchukuliwa kwa meli ya MV.Wankyo ikiwemo;

i.Kuwasiliana na Mmiliki wa meli ili kupata taarifa rasmi kuhusu tukio hilo;

ii.Kumsimamisha nahodha wa meli ya MV. Wankyo kuendelea kutoa huduma kama nahodha mpaka uchunguzi utakapo kamilika; na

iiii.Kuzifanyia ukaguzi meli zote mbili ambapo ukaguzi kwa Meli ya MV.Wankyo ili kujua uwezo wa utendaji kazi katika mifumo ya meli ikiwemo mfumo wa kuongozea na Meli ya MV.Kyone ili kubaini iwapo imepata athari zozote.

"TASAC inaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu tukio hilo na itatoa taarifa kwa umma mara baada ya kukamilika kwa uchunguzi huo.

"Aidha, TASAC inatoa wito kwa wadau wote wa usafiri majini kuhakikisha wanazingatia taratibu za usalama zilizowekwa katika uendeshaji wa vyombo vya usafiri majini ili kuepusha madhara yanayoweza kutokea kwa binadamu, mizigo, meli pamoja na uharibifu wa mazingira ya majini."

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news