Ujio wa The Friendship Run between India and Tanzania with Milind Soman

DAR ES SALAAM-Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa India nchini Tanzania, Mhe. Binaya Pradhan.

Pamoja na mambo mengine, viongozi hao wamejadili kuhusu tukio la mbio za pamoja za kudumisha ushirikiano kati ya Tanzania na India la The Friendship Run between India and Tanzania with Milind Soman"linalotarajia kufanyika jijini Dar es Salaam kati ya tarehe 30 na 31 Desemba,2023.

Akizungumza kuhusu tukio hilo Desemba 5, 2023 Mhe. Ndumbaro amesema Serikali ya India imeomba ushirikiano na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo ili kufanikisha tukio hilo ambalo litahudhuriwa na mwanariadha maarufu kutoka nchini India Milind Soman.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Bi.Neema Msitha, Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Dkt.Kiagho Kilonzo na Makamu wa rais wa Shirikisho la Riadha Tanzania, William Kallaghe.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news