Wadau wa Sekta ya Elimu washauriwa kuchangia maendeleo ya elimu kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa

DAR ES SALAAM-Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imekuwa mstari wa mbele katika kutekeleza, na kusimamia Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ikiwemo kusimamia upatikanaji wa elimu bora na kwa usawa kote nchini pamoja na uboreshaji wa miundombinu ya kujifunzia na kufundishia.
Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Elimu Tanzania Dkt. Erasmus Kipesha akitoa Elimu kwa mdau aliyetembelea banda la TEA wakati wa maonesho ya miaka 50 ya Baraza la Mitihani la Tanzania yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam viwanja vya Mnazi Mmoja.

Katika kufanikisha utekelezaji wa malengo haya, Serikali imeendelea kufanya maboresho makubwa katika sekta ya Elimu kuanzia elimu ya awali, msingi, sekondari hadi vyuo vikuu. Maboresho na mageuzi haya yanahitaji rasilimali na nguvu kazi kutoka kwa wadau mbalimbali ili kuunga mkono jitihada za Serikali za kuboresha sekta ya sekta ya Elimu.
Afisa Miradi kutoka TEA Bi. Mwafatma Mohamed akitoa Elimu kuhusu kazi zinazotekelezwa na TEA katika Maonesho ya miaka 50 ya Baraza la Mitihani la Tanzania Jijini Dar es Salaam.

Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) inalo jukumu la kuhamasisha uchangiaji maendeleo ya Elimu kote nchini ambapo, kwa mujibu wa Sheria ya Mfuko wa Elimu, Namba 8 ya mwaka 2001 sehemu ya 12 (1) (a) na (b) mchangiaji ni mtu yeyote anayetoa mchango wa pesa, bidhaa, au huduma kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa au kutekeleza mradi kwa uratibu wa Mfuko huo wa Elimu.
Hamza Hassan (Mwenye tisheti nyeupe) Afisa Utafutaji Rasilimali akifafanua jambo kwa mdau wa Elimu aliyetembelea banda la TEA katika Maonesho ya miaka 50 ya Baraza la Mitihani la Tanzania Jijini Dar es Salaam.

Aidha, mchangiaji anaweza kuwa mtu yeyote anayetoa udhamini au ruzuku kwa wanafunzi mbali na watoto wake, familia yake au mwajiri wake, kwa lengo la kuwasaidia kuendelea na elimu kwenye ngazi ya sekondari au elimu ya juu ambapo udhamini huo atautoa kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa.
Kaimu Mkurugenzi Utafutaji Rasilimali na Usimamizi wa Miradi Masozi Nyirenda akitoa elimu kwa wadau waliotembelea banda la TEA wakati wa maonesho ya miaka 50 ya Baraza la Mitihani la Tanzania yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam viwanja vya Mnazi Mmoja.

Wadau na wachangiaji wa maendeleo ya Elimu kote nchini wanahimizwa kutoa michango yao kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa ili waweze kutangazwa na kutambuliwa kitaifa, ambapo mchangiaji huandikwa katika rejesta ya kudumu ya wachangiaji wa elimu.
Kaimu Mkurugenzi Utafutaji Rasilimali na Usimamizi wa Miradi Masozi Nyirenda akitoa elimu kwa wadau waliotembelea banda la TEA wakati wa maonesho ya miaka 50 ya Baraza la Mitihani la Tanzania yaliyofanyika Jijini Dar es Salaam viwanja vya Mnazi Mmoja.

Faida nyingine ya kuchangia kupitia Mfuko wa Elimu wa Taifa ni kupata Hati ya Utambuzi wa Uchangiaji wa Elimu (Certificate of Educational Appreciation ambapo mchangiaji anaweza kuitumia kuomba nafuu ya kodi kutoka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kwa mujibu wa Kifungu cha 16 (1) cha Sheria ya Kodi ya Mapato Sura 332 marejeo ya mwaka 2019.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news