Washiriki COP28 UAE wamejigharamia wenyewe-Serikali

DUBAI-Serikali imesema idadi kubwa ya watanzania wanaoshiriki Mkutano wa 28 wa Nchi Wanachama wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi - COP 28 wanashiriki kwa gharama zao wenyewe kutokana na mwamko katika masuala ya mazingira na mabadiliko ya tabianchi.
Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Vijana wanaojishughulisha na masuala ya mazingira nchini wakati alipotembelea Banda la Maonesho la Tanzania kwenye viwanja vya Expo Dubai wakati wa Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28), UAE tarehe 2 Desemba, 2023.

Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) imesema katika taarifa kwa vyombo vya habari kuwa baadhi ya washiriki kutoka Wizara na Taasisi za Serikali wamefadhiliwa na Mashirika ya Kimataifa wakati washiriki kutoka Sekta Binafsi, Taasisi za kiraia, vijana na watoto wamejigharamia.

Mkutano huo umelioanza Novemba 30 unatarajia kuendelea hadi Disemba 12 2023 huko Dubai katika Umoja wa Falme za Kiarabu ambapo washiriki wakiwemo wakuu wa nchi na Serikali zaidi ya 31,000 kutoka nchi takriban 190 wanahudhuria. Rais Samia Suluhu Hassan pia anashiriki Mkutano huo.

“Ikumbukwe kwamba jitihada za kukabiliana na mabadiliko ya Tabianchi zinahusisha wadau mbalimbali ikiwemo Serikali, Asasi za Kiraia, Sekta Binafsi, Vijana na Watoto, hivyo, Idadi kubwa ya Watanzania ilionyesha nia ya kushirki katika mkutano huo wa kimataifa,” imesema taarifa ya serikali.

Jumla ya Watanzania 763 walijiandikisha kwa nia ya kushiriki. Kati ya idadi hiyo Watanzania 391 walijiandikisha kutoka Wizara na Taasisi za Serikali, wakati 372 walijiandikisha kutoka Mashirika yasiyokuwa ya kiserikali, Sekta binafsi, Vijana na Watoto.

Hata hivyo idadi ya Watanzania wanaoshiriki kutoka Serikalini ni 66 ambapo 56 wanatoka Tanzania Bara na 10 kutoka Zanzibar ambayo ni sawa na asilimia 8.7 ya watanzania waliojiandikisha.

Aidha, sehemu kubwa ya washiriki inatoka katika Sekta Binafsi, Mashirika yasiyo ya Kiserikali pamoja na vijana na Watoto ambayo ni 340, sawa na asilimia 91.3.

Diramakini

DIRAMAKINI is Tanzanian news media house established to play role in shaping the global agenda through telling true stories by delivering quick and in-depth.Our readers trust our coverage of the issues that matter most to them. Our agenda-setting journalism attracts. Contact us on diramakini@gmail.com OR +255 719 254 464.

Post a Comment

Previous Post Next Post

International news